November 21, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wahitimu 417 kutunikiwa vyetu ITA

 

CHUO cha Kodi (ITA), kinatarajia kuwatunuku vyeti wahitimu 417, wa kozi mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2023/2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema wanatarajia kutunuku vyeti kwa wahitimu 417 wa kozi mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Hayo yamesema leo tarehe 20 Novemba 2024 na Mkuu wa Chuo hich,o Profesa Isaya Jairo wakati anazungumza na waandishi wa habari chuoni hapo jijini Dar es Salaam amesema kuwa vyeti hivyo vitatolewa siku ya mahafali ya chuo hicho yatakayofanyika tarehe 22 Novemba, mwaka huu.

Prof. Jairo amesema kuwa kwenye mahafali hayo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa fedha Dk. Mwigulu Nchemba na atatunuku wanafunzi wa vyeti, Stashahada,Shahada na Stashahada ya Uzamili.

“Pamoja na kutunuku vyeti pia atatoa zawadi kwa wanafunzi wanaobaki chuoni hapa ili kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.Katika idadi hiyo wanaume ni 236 na wanawake 181 ambapo195 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha wa Afrika Mashariki(EACFF),” amesema Prof. Jairo.

Ameongeza,”Wahitimu 28 watatunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM),
61 watatunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na kodi (DCTM), 119 watatunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na Wahitimu 14 watatunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT),”

Amesema kuwa Chuo hicho kinajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa wamu ya Tano wa Chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo kwa njia ya kisasa yaani kidijitali.

“Tayari maandalizi ya kutoa elimu masafa kwa njia ya mtandao yameanza na yanaendelea vizuri hivyo itasaidia kupunguza gharama kwa wanafunzi walioko mikoani na kuongeza idadi ya wahitimu kwani mwanafunzi hayakuwa na ulazima wa kusafiri kuja chuo bali kila kitu atapata mtandaoni,” amesema Prof. Jairo

Profesa Jairo amesema pamoja na jukumu kubwa la kutoa mafunzo kwa Watumishi wa TRA, Chuo cha Kodi vilevile kinatoa mafunzo na ushauri
elekezi kwa wadau wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA)na mamlaka zingine za Mapato Afrika kama vile Sudan, Botswana na Somalia.

Jairo alitumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii kuwa kufanyika kwa mahafali ni fursa nzuri ya kuwapongeza wahitimu pamoja na kutathmini mafanikio na shughuli ambazo zinafanywa na Chuo. Pamoja na kuwaalika wageni kutoka Mataifa mbalimbali ambao ni wadau na washirika katika maendeleo ya taaluma ya forodha na kodi ili kuvutia fursa za uwekezaji.

About The Author