WADAU wa maendeleo wameombwa kuendelea kusaidia sekta ya kilimo nchiniTanzania, hasa kwa kundi la vijana na wanawake ili kuhakikisha wanaleta mchangokatika sekta hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Baku, Azerbaijan … (endelea).
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Amina Khamis Shaaban wakati akiongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano kujadili fursa zauwekezaji zilizopo katika Sekta ya Kilimo na namna ya kutafuta rasilimali fedha zakukabiliana na uhimilivu wa mabadiliko ya Tabianchi.
Mkutano huo uliofanyika Pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama waUmoja wa Mataifa wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaoendeleajijini Baku, Azerbaijan na kuandaliwa na Wizara ya Kilimo na Shirika Care Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu, Amina amesema upatikanaji wa ufadhili endelevu na wa mudamrefu bado ni changamoto inayoendelea kwa nchi zinazoendelea hivyo ni wakatimuafaka kwa wadau kusaidia katika sekta hiyo muhimu ili kupata rasilimali fedha zakutosha ili kuleta mageuzi.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu Amina ameshukuru Serikali ya Norway kwa kuendeleakuiunga mkono Tanzania katika sekta ya kilimo kinachohimili athari za mabadiliko yatabianchi.
Amebainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka waziajenda na vipaumbele vya kuleta mabadiliko katika kilimo kwa lengo la kuongezaualishaji wa mazao.
Amefafanua kuwa mikakati na sera zinaeleza kuwa ili kukuza ujuzi kwa wakulimainapaswa kutoa motisha kwa ushiriki wa sekta binafsi, kuimarisha minyororo yathamani na shughuli za uzalishaji, kuhakikisha usalama wa chakula na uwekezaji wamiundombinu.
“Tanzania imejikita katika kuhakikisha usalama wa chakula huku ikijenga mifumojumuishi zaidi, endelevu, yenye lishe na ustahimilivu. Katika COP 29 hatatunapoangazia ajenda tofauti, bado tunahimiza washirika tofauti kuendeleza mifumoya chakula na hatua za hali ya hewa katika muktadha wao wa kipekee,” amesema.
ZINAZOFANANA
Wakazi wa Mdundwaro waishukuru TASAF kuwajengea nyumba ya watumishi
Tanzania yakosa Bil 9.3 za nyama
Tanzania yang’ara Uimara wa kiuchumi: IMF yathibitisha Tanzania kuimalika