MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu tarehe 16 Disemba 2024 kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Salamaan Dk. Abdi Hirsi katika inayomkabili mahakamani hapo ya kughushi nyaraka ili kujipatia kibali cha uwekezaji asichostahili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Leo tarehe 20 Novemba 2024, Dk. Hirsi anayetetewa na Wakili Juma Nassoro alijitetea juu ya tuhuma hizo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rahim Mushi.
Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Tuamaini Mafuru.
Dk. Hirsi anadaiwa kughushi nyaraka za uwekezaji na kupatiwa kibali daraja la chini la uwekezaji ili alipe kidogo ilhali hakustahili kulipa kiwango hicho.
ZINAZOFANANA
Washtakiwa 57 wa uhaini waanza kuachiliwa
Wahamiaji haramu 14 wakamatwa Mwanza
Ripoti yetu kuhusu Tanzania imezingatia weledi – CCN