MBUNGE wa Tanga Mjini Ummy Mwalimu ametambua na kupongeza jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Maji chini ya Waziri Jumaa Aweso katika kuhakikisha upatikanaji wa maji mkoani Tanga unakuwa wa ufanisi mkubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).
Ummy ametoa pongezi hizo siku ya Jumanne Novemba 19, 2024 wakati wa ziara ya Waziri Aweso katika Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Huduma ya Maji Tanga Kupitia Hatifungani ya Kijani (Kijanibond) unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA)
Ummy amesema kuwa mkoa wa Tanga kuliahidiwa kutatuliwa changamoto tatu za maji ambazokukatikakatika maji, bili kubwa za maji, na majitaka hasa kwenye barabara za namba, hata hivyo ameridhishwa na mambo hayo matatu kuanza kutekelezwa.
Aidha Waziri Ummy ameisifu TANGAUWASA kwa mradi wa hatifungani wa thamani ya Sh. 53.12 bilioni ambao umewawezesha upatikanaji wa maji kwa kutumia pesa za wawekezaji wananchi akiwamo yeye mwenyewe.
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya mradi huo, Waziri Aweso amesema kuwa mkoa wa Tanga umekuwa mfano Tanzania na duniani kote kwa kuwa na taasisi ya umma kujiendesha kibiashara akiashiria taasisi ya TangaUWASA kutekeleza mradi wa maji wa hatifungani.
Amesema kwa kuwa fedha za mradi huu zipo basi nguvu inahitajika ili ukamilike kwa asilimia 100.
Aidha ameiomba taasisi hiyo kuendeleza uaminifu wa kulipa gawio stahiki kwa wawekezaji katika hatifungani ya maji kwani ni mradi unaotekelezwa kwa kutumia fedha za wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amesema kuwa jitihada kubwa zimefanyika kuboresha huduma ya maji safi na salama mkoani Tanga ikiwamo wananchi kufungiwa mita za luku za maji (Mita za malipo ya kabla) ili kuondokana na changamoto ya ubambikiziaji wa bili za maji.
Aidha amesema kuwa changamoto ya majitaka Tanga jiji litabaki kuwa historia kwakuwa tayari kuna kiasi cha fedha kimetengwa kuhakikisha miundombinu ya majitaka inakwenda kuboreshwa.
Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Huduma ya Maji Tanga Kupitia Hatifungani umetoa fursa kwa jamii kushiriki katika uwekezaji kupitia ununuzi wa hisa (bonds) hivyo kufanikisha upatikanaji wa fedha zitakazotumika katika utekelezaji wake.
Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu ukilenga kuboresha miundombinu katika kituo cha kuzalisha na kusambaza maji cha Mowe, kuboresha miundombinu ya mabomba ya kusambazia maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga, Mji wa Muheza, Pangani na Mkinga, kufunga Mita za Malipo ya Kabla (Smart Prepaid Water meters) kwa wateja 10,000 na kuendeleza jitihada za utunzaji wa vyanzo vya maji.
Mapema mwezi Februari, 2024 Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdor Mpango alizundua rasmi Dirisha la uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya TANGA UWASA, ambapo makusanyo ya mauzo hayo yalizidi lengo kwa asilimia 103 ambapo TANGA UWASA ilifanikiwa kukusanya Shilingi za Kitanzania Bilioni 54.72 ambapo lengo halisia lilikuwa ni kukusanya Shilingi Bilioni 53.12.
ZINAZOFANANA
Mmiliki wa jengo lililoporomoka K/koo atafutwe – Majaliwa
Waliokufa ajali K’koo wafikia 13, Rais aagiza uchunguzi ufanyike
RC Chalamila tunaendelea kuokoa majeruhi K’koo kwa ustadi mkubwa