KITUO cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha Mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya PPPC yamefanyika leo Novemba 11, 2024 katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam. Katika mambo ambayo yamejadiliwa ni pamoja umuhimu wa kutumia PPP katika utekelezaji wa Mipango ya Taifa ya Maendeleo ya nchi, muundo wa kisheria na Kitaasisi katika utekelezaji wa program ya PPP Tanzania. Mambo mengine ambayo yamejadiliwa ni pamoja na dhana ya PPP na Orodha ya Miradi ya PPP iliyoandaliwa chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Sloti ya 777 Super Strike inakupa nafasi ya malipo x243 Cheza Sloti ya 100 Super Icy Ushinde Mikwanja Leo