December 22, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

GF Vehicle yashinda Tuzo ya Rais kwa uunganishaji magari nchini

 

KIWANDA cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimeibuka mshindi kwanza kwa makampuni ya Kati nchini wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) zilizofanyika jijini Dar es salaam za mwaka 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hilyo Meneja mkuu wa Kiwanda hicho , Ezra Mereng amesema anawapongeza wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya wao kukidhi Ubora katika uzalishaji wa magari bila wao wasingweweza kufanikiwa katika ushindi na tuzo hii ni ya 2 kwa kampuni ya GFA.

Salman Karmali, mkurugenzi wa Masoko na Mawasilianao wa Kampuni hiyo, alisema wao kama kampuni wanashukuru tuzo hiyo ni dalili mzuri kwani kiwanda hicho cha kuunganisha magari nchini Ndio kiwanda cha kwanza  hapa Tanzania kunganisha magari makubwa  pia tunajivunia  kuwa waongoza njia katika sekta ya Usafirishaji.

Karmali alisema GFA ni kiwanda kikubwa kilichopo kibaha mkoani Pwani na kutokana na mafanikio wanaingia katika hatua ya pili ya upanuzi na uzalishaji ambapo wanatarajia katika upanuzi huu  awamu ya pili kutengeneza magari 10(trucks) kwa siku kutoka magari 4 ambayo kwa itaunganisha magari makubwa na madogo.

Pia mkakati ni kulifikia soko la ndani la nje ili kuliiingizia Taifa pesa za kigeni kwa kuuza magari katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika watumie bidhaa kutoka Tanzania jambo ambalo hapo zamani halikuzoeleka miongoni mwa magari hayo ni FAW,HONG YAN na FOLAND

Tunaipongeza serikali kuweka mazingira mazuri hasa sheria ya Local Content kuwawezesha Watanzania kufanya kazi mbalimbali na kutoa huduma migodini na miradi ya serikali hali iliyokuza vipato vya Watanzania wengi na kumudu kununua magari kutoka kiwandani kwetu alimaliza Karmali.

About The Author

error: Content is protected !!