SERENGETI Breweries Limited (SBL) imeibuka kuwa mzalishaji bora wa pombe kali kwenye Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora (PMAYA), zilizofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki, Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Tuzo za PMAYA, ambazo ni miongoni mwa heshima za juu kabisa kwa wazalishaji nchini Tanzania, zimeundwa kutambua na kuhamasisha ubora kwa wazalishaji katika sekta mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, aliipongeza timu nzima ya SBL kwa juhudi zao na kusisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kuendelea kuboresha ubora wa bidhaa zake huku ikichangia katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Alisema, “Tumejizatiti kuunda bidhaa zinazozingatia viwango vya ubora na uendelevu ili kukidhi na kuvuka viwango vya sekta, na kuweka kampuni katika nafasi ya pekee kama mdau muhimu katika sekta ya uzalishaji nchini Tanzania.”
Mgeni rasmi, Makamu wa Raisi Dk. Philip Mpango kwa niaba ya Raisi Dk. Samia Suluhu Hassan, alieleza kuwa serikali imeimarisha miundombinu ya barabara na bandari ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa nje na ndani ya nchi, kwa lengo la kusaidia mafanikio ya sekta ya viwanda. Aidha, aliwahimiza wazalishaji kuongeza juhudi katika uzalishaji na kuongeza bidhaa za katikati (intermediate goods) ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.
SBL imeahidi kuendelea kuiunga mkono uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza zaidi, hususan katika sekta ya kilimo. Kwa sasa, zaidi ya 75% ya malighafi inayotumika katika uzalishaji wa bia zake inapatikana nchini, na hivyo kunufaisha moja kwa moja wakulima wa Kitanzania na kuimarisha mnyororo wa ugavi wa kilimo nchini.
Kwa kutilia mkazo ununuzi wa ndani, SBL inalenga sio tu kupunguza utegemezi wa uagizaji, bali pia kuwawezesha jamii za vijijini, kuunda ajira, na kuendeleza kilimo endelevu. Uwekezaji huu unaendana na dhamira kuu ya SBL ya kusaidia viwanda vya ndani, kukuza uchumi, na kuchangia kujitosheleza kwa Tanzania katika rasilimali muhimu za uzalishaji.
ZINAZOFANANA
Black Gold kasino mambo iko huku
Meridianbet yatoa msaada wa jezi Kimara
All Aces Poker ndio mchongo kwa sasa