December 14, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Chama tawala Botswana chaangushwa vibaya

Duma Boko

 

WAPIGAKURA nchini Botswana wamekikataa chama tawala cha muda mrefu cha nchi hiyo (BDP) katika matokeo ambayo yanaashiria tetemeko la ardhi la kisiasa katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa almasi kusini mwa Afrika. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa, GABORONE, Botswana … (endelea).

BDP – Chama cha Kidemokrasia cha Botswana – kilichokuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1966 – kimeshinda kiti kimoja pekee cha ubunge kufikia mapema Ijumaa asubuhi. Inaonekana nafasi yake kuchukuliwa na Umbrella for Democratic Change yaani Mwavuli wa Mabadiliko ya Demokrasia (UDC).

Rais Mokgweetsi Masisi amekubali kushindwa, akisema ni wazi kuwa chama chake cha BDP kimeshindwa “pakubwa”.

Licha ya kusimamia mabadiliko makubwa nchini Botswana, ukuaji duni wa uchumi wa hivi karibuni na ukosefu mkubwa wa ajira ulidhoofisha umaarufu wa BDP.

“Nitang’atuka kwa heshima na kushiriki katika mchakato mzuri wa kukabidhi mamlaka kabla ya kuapishwa,” amesema Masisi katika mkutano na waandishi wa habari asubuhi ya leo Ijumaa.

Amewataka wafuasi wake kuwa watulivu na kuiunga mkono serikali mpya.

UDC, inayoongozwa na wakili wa haki za binadamu Duma Boko, imeshinda viti 25, kulingana na hesabu za mapema. Chama hicho kinatarajiwa kupata Zaidi ya kizingiti cha viti 31 ili kuwa na wingi wa wabunge.

Chama cha Botswana Patriotic Front (BPF) kinachoungwa mkono na Rais wa zamani Ian Khama, kimepata viti vitano huku Chama cha Botswana Congress Party (BCP) hadi sasa kimepata viti saba.

Chama chenye wingi wa wabunge ndicho kinatarajiwa kuunda serikali. Boko yuko mbioni kuwa mkuu wa nchi mara baada ya Bunge kukutana kwa mara ya kwanza.

Wafuasi wa UDC wamekuwa wakisherehekea katika mji mkuu Gaborone na mae

About The Author

error: Content is protected !!