WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya kazi kubwa sana katika uwekezaji kwenye Miundombinu ya Elimu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Busega, Mwanza … (endelea).
Waziri Aweso ameyasema hayo baada ya kuzindua mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Kata ya Mwanuzi yenye madarasa nane, jengo la Utawala, Maabara tatu,vyoo kumi, chumba cha kompyuta Maktaba na kichomea taka.
Mradi huu umetumia kiashi cha shilingi 584,280,028
Akizungumza na wazazi na wanafunzi Waziri Aweso amewaasa kusoma kwa bidii kwani elimu ndio mkombozi wa jamii ya Mtanzania.
Tukio hili limefayika Wilayani Meatu leo tarehe 27 octoba 2024 akiendelea na ziara maalumu inayohusisha kutembelea, kuweka mawe ya msingi, kukagua na kuzindua Miradi ya Maendeleo ya sekta mbalimbali sambamba na kuzungumza na wananchi kwaniaba ya Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ZINAZOFANANA
Mradi wa Nishati Safi wa EWURA kupunguza madhara ya kuni kwa jamii
TCC yaibuka kidedea tuzo za PMAYA Dar
Wahariri wamparura Waziri Silaa kwa kuwakacha