Swali la umeifanyia nini Tanzania ndilo lililobeba ajenda kuu katika baraza la vijana la Samia Love lililofanyika jijini Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).
Baraza hilo, lililokutanisha mamia ya kundi la vijana limekuwa kielelezo cha tafsiri ya kabla hujaomba onyesha ulichonacho.
Hilo ni kutokana na hotuba na mawasilisho ya vijana mbalimbali katika tukio hilo, walioeleza na kuonyesha mchango wao kwa taifa, badala ya kulalamika.
Walikuwepo waliopoteza mwelekeo wa elimu na baadaye kuibuka vinara wa ubunifu, hivyo kuzalisha maelfu ya ajira, kadhalika wapo waliokuwa kielelezo cha usemi wa vijana ndiyo msingi wa fursa kwa wengine.
Kama unasoma kusubiri fursa kutoka kwa Serikali, baraza hilo limetoa jawabu sahihi la namna kijana anavyopaswa kuenenda ili anufaishwe na mazingira anayoishi.
ZINAZOFANANA
Mil.600 zatengwa kupeleka umeme Kijiji cha Ijinga – Magu
Wakazi wa Mdundwaro waishukuru TASAF kuwajengea nyumba ya watumishi
Tanzania yakosa Bil 9.3 za nyama