October 18, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama yasitisha kuondolewa kwa Gachagua ofisini

 

MAHAKAMA Kuu katika Jamhuri ya Kenya, imesitisha utekelezwaji wa azimio la Seneti la kuidhinisha mashtaka ya kumuondoa madarakani Rigathi Gachagua. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa muda mfupi tu baada ya Bunge la Kitaifa kuafiki uteuzi wa Kithure Kindiki kuwa Naibu wa Rais baada ya Rais William Ruto kuwasilisha jina lake kwenye bunge hilo.

Hapo jana Maseneta nchini humo waliidhinisha mashtaka 5 kati ya 11 dhidi ya Gachagua na kumuondoa ofisini.

Gachagua alikosa kufika mbele ya maseneta kujitetea baada ya mawakili wake kusema alipatwa na ”maumivu makali ya kifua” na kulazimika kulazwa hospitalini.

Uamuzi uliotolewa na Jaji E.C. Mwita umezuia kutekelezwa kwa azimio hilo la seneti na pia kuzuia rais kumteua mtu kuichukua nafasi hiyo hadi tarehe 24 mwezi huu hadi kesi hiyo sikilizwe na jopo la majaji watakaoteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Hata hivyo tayari rais amependekeza jina la Kithure Kindiki kuichukua nafasi ya Gachagua na bunge la taifa kuafiki uteuzi wake.

About The Author