December 25, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Israel yaanza uvamizi wa ardhini kusini mwa Lebanon

 

ISRAEL imeanza operesheni ya ardhini kusini mwa Lebanon, kwa mashambulizi madogo, ya ndani na yanayolenga maeneo ya Hezbollah, jeshi la Israel limesema. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Leo, vyombo vya habari vya kimataifa vimechapisha picha zinazoonesha msururu wa vifaru na magari ya kijeshi yakielekea Lebabon.

Akizungumza katika kipindi cha BBC Radio 4 cha leo Jumanne, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel, Luteni Kanali Peter Lerner, amesema Hezbollah ina vituo vya mapigano kusini mwa Lebanon, ambavyo vilikusudiwa kutumika kuishambulia Israel kama Hamas ilivyofanya tarehe 07 Oktoba 2023, yaliyofanywa na mwanamgambo wa Hamas.

“Ndio maana jeshi la Israeli lilihamia huko na kufanya mashambulizi usiku kucha ili kuvunja miundombinu hiyo,” amesema.

Kanali Lerner amesema tofauti kati ya vita vya sasa na kile kinachoendelea ukanda wa Gaza ni kuivunja Hamas kama mamlaka inayotawala eneo hilo na kwamba nchini Lebanon operesheni yake inalenga zaidi vitisho vinavyotolewa kwa raia wa Israeli.

Alipoulizwa mbona Israel imevamia nchi huru, Kanali Lerner amesema Hezbollah ilianza kuichokoza Israel tarehe 08 Oktoba mwaka jana na kuwasambaratisha maelfu ya Waisraeli kwa roketi mpakani.

Amesema hatua yake ya kujibu uchokozi huo ni kujaribu kuwarudisha watu wao nyumbani salama.
“Hakuna mpango wa kuikalia Lebanon, mpango ni kuvunja miundombinu ambayo Hezbollah iliianzisha kuua Waisraeli,” Lerner amesema.

About The Author

error: Content is protected !!