October 16, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Hezbollah wajibu mapigo

 

KUNDI la wapiganaji wa Hizbollah, nchini Lebanon limejibu mapigo baada ya Israel kuyashambulia makao makuu yake huko Hezbollah, Beirut. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endela).

Israel ilifanya mashambulizi kadhaa kwenye makao makuu ya kundi hilo na kwamba mkuu wa Hezbolla, Hassan Nasrallah ndiye aliyekuwa akilengwa.

Jeshi la Israel limesema pia kuwa limemuua kamanda wa Hezbollah Muhammad Ali Ismail na naibu wake Hossein Ahmed Ismail kusini mwa Lebanon.

Lakini kundi la Hezbollah limetangaza kuwa kiongozi wake yuko salama na kwamba wamejibu mashambulizi kwa kurusha makombora kuelekea mji wa kaskazini mwa Israel wa Safed.

Makabiliano hayo yanajiri baada Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuihutubia hapo jana hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa na kuapa kupigana kuwalinda watu wake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amesema anaunga mkono mpango wa usitishwaji mapigano huko Lebanon na kuonya kuwa eneo la Mashariki ya Kati liko hatarini kutumbukia katika janga kubwa.

About The Author