JUMLA ya viongozi wa kimila 103 kutoka makundi ya watu wa asili (VEG-IP) wanaopitiwa na Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika ya Mashariki (EACOP) wamenolewa na kupewa elimu namba mradi huo utatekelezwa kwa kuheshimu mila na tamaduni zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha …(endelea).
Viongozi hao wamepatiwa matunzo hayo katika mkutano wa robo ya tatu wa mwaka ikiwa ni utekelezaji wa sheria za kimataifa inayotaka haki za watu hasa wale wa asili zinaheshimiwa pale inapotokea asili, urithi, rasilimali na tamaduni zao kuguswa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimishwa kwa mkutano huo mwishoni wa wiki jijini Arusha, Mkuu wa Idara ya Ushirikishwaji jamii Mradi wa EACOP upande wa Tanzania, Fatuma Msumi alisema mkutano huo umeangazia zaidi maendeleo ya mradi ulipofikia, mipango ya baadaye sambamba na kutoa elimu kwa jamii hiyo.
“Mkutano wa leo umewakutanisha viongozi wa kimila 103 kutoka makabila ya wataturu, Wamasai, wakiha, wabarbei kutoka Vijiji 29, Halmashauri 9, na Wilaya 7 zikiwemo Handeni TC, Handeni DC, Kilindi, Simanjiro, Kiteto, Kondoa TC, Kondoa DC, Hanang na Igunga,” alisema Msumi.
Msumi alieleza kuwa EACOP inajivunia kuona mradi unatekelezwa bila malalamiko yoyote katika jamii inayoguswa na kuheshimu milana tamaduni za za jamiii husika bila kuathiri haki zao za msingi.
Aidha, Msumi alisema Mkutano huu ulikuwa na mada mbalimbali zikiwemo taarifa ya mradi kwa jumla, taarifa ya ujenzi wa bomba, taarifa ya upataji ardhi, taarifa za hatua zinazolenga kurejesha na kuboresha maisha ya waguswa sambamba na taarifa za Haki za Binadamu na Usimamizi wa Malalamiko.
Kwa Upande mjumbe wa Timu ya Usimamizi wa EACOP kutoka Wizara ya Nishati, Benson Lukuta alisema mkutano huu umeonesha namna EACOP inavyoshirikiana kwa karibu na jamii za asili kwa kutoa fursa ya kujadiliana nao katika mambo yanayowaguswa katika utekelezaji wa mradi huo huku kipaumbele ikiwa ni kuzingatia haki, mila, tamaduni na desturi ya maisha yao.
“Eacop imeendelea kutekeleza kwa vitendo Ushirikishwaji wa wananchi katika miradi endelevu ya kimkakti (Local Content) kwa kuwapa vipaumbele vya ajira wazawa wanaoishi ulipopita mradi na hivyo kuchochea maendeleo yatakayokuza uchumi wa Taifa,” alisema Lukuta.
Naye kiongozi wa kabila ya Wabarbaig James Gejaru mbali ya kuishukuru EACOP kwa kuwapa kipaumbele jamii za pembezoni alisema EACOP imeonesha kuelewa na kuheshimu utamaduni wao, hasa kwa kupunguza njia katika eneo lenye kaburi la mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila hilo.
Alisema ushirikishwaji wa viongozi wa kimila kwenye mradi huo ni wazi EACOP imejizatiti katika utekelezaji wa mradi unaowajibika na unaoshirikisha sambamba na kuheshimu haki na urithi wa kitamaduni wa wazawa,” alisema Gejaru.
EACOP kujizatiti katika utekelezaji wa mradi unaowajibika na unaoshirikisha, kuheshimu haki na urithi wa kitamaduni wa wazawa.
Naye Mwenyekiti wa Jamii ya watatoga Shindaria Kishaida aliipongeza EACOP kwa hatua mbalimbali inayochukuwa ikiwemo kuwashirikisha hatua za mradi unavyoendelea kuanzia awali kwani inawapa uwelewa wa pamoja jamii hizo kuhusu mradi na namna utakavyowanufaisha.
“Kazi yetu kubwa ni kuelimisha jamii zetu za kifugaji kuhusiana na maendeleo ya mradi sambamba na fursa za ajira zinazopatikana ikiwemo mafunzo kwa vijana wetu ambayo wanaandaliwa kuwa miongoni mwa wataalam kutoka jamii za kifugaji wataohudumu katika ujenzi wa mradi,” alisema Kishaida.
EACOP ni mradi unaohusisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Kijiji cha Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, ulio na urefu wa kilomita 1,443, ambapo kati ya hizo, kilomita 1,147 zipo nchini Tanzania na kilomita 296 nchini Uganda.
Wanahisa wa EACOP ni TotalEnergies yenye wasilimia 62, Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) yakimiliki asilimia 15 kila moja na kampuni ya mafuta ya Kichina (CNOOC) ikiwa na asilimia nane.
ZINAZOFANANA
Polisi: Waharifu 2024 wapungua mkoani Songwe
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Mil.600 zatengwa kupeleka umeme Kijiji cha Ijinga – Magu