GOLIKIPA wa klabu ya Simba ya Tanzania, Aishi Manula, alipigwa na polisi baada ya kumalizika kwa mchezo mgumu wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF uliochezwa jana Jumapili nchini Libya. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa DW … (endelea).
Afisa mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa alisema aliona Manula akishambuliwa bila ya sababu yoyote na wachezaji wengine walirushiwa chupa na vitu vingine, hali iliyomtisha sana.
Manula hakuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza mchezo huo.
Afisa huyo aidha amesema, alishuhudia wachezaji wa Ahly wakiwashambulia waamuzi wa mechi hiyo na wasaidizi wao.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili dhidi ya Al Ahly ulimalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Tripoli uliofurika mashabiki ambao muda wote walikuwa wakiwarushia wachezaji wa Simba chupa za plastiki.
ZINAZOFANANA
Jogoo Veterean yafurahia ujio wa Meridianbet
Wikendi inaanza kwa kubashiri na Meridianbet leo
Leo hii una nafasi ya kuondoka bingwa ukiwa na Meridianbet