WANANCHI wa kata ya Ntobeye Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera wameonywa na Jeshi la Polisi kujichukulia sheria mkoani na kufanya mauaji ya watu kwa imani za kishirikina wilayani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngara Mrakibu wa Polisi, SP William Solla wakati akiongea na wananchi wa kata hiyo ambapo amebainisha kuwa katika siku za hivi karibu kumejitokeza tabia za watu kujichukulia sheria mkononi na kufanya mauaji kitendo ambacho ni kinyume na taratibu za sheria huku akisema kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi litawakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Aidha SP Solla amebainisha kuwa zipo njia sahihi ambazo wananchi wanapaswa kuzifuata endapo wananchangamoto zao kuliko kujichukulia sheria mkononi na kupoteza uhai wa watu wasio na hatia.
Vile vile amewaomba wananchi hao kutambua kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kuwahudumia na kuhakikisha wako salama na mali zao huku akisisitiza kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Jeshi hilo liwachukulie hatua za kisheria watakao bainika katika vitendo vya uhalifu.
ZINAZOFANANA
Polisi: Waharifu 2024 wapungua mkoani Songwe
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Mil.600 zatengwa kupeleka umeme Kijiji cha Ijinga – Magu