WATU 11 wamepoteza maisha na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya A-N Coach lenye namba ya usajili T282 CXT kupata ajali katika eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Ijumaa, Septemba 6, 2024 baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka wakati likilikwepa lori, kisha kutumbukia mtaroni.
Mganga wa Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Chunya, Dk. Darson Andrew amethibitisha kupokea idadi ya hiyo na vifo huku akieleza kati ya majeruhi 44 wanne wana hali mbaya na watapewa rufaa kupelekwa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
ZINAZOFANANA
TRA yazindua ofisi ya walipa kodi binafsi
Mwenge wa uhuru wazindua mradi wa maji Kahangara -Magu
DC: Ilala hali ni shwari uandikishaji