MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Dk. Andrew Komba amesema taasisi hiyo imejipanga kuongeza uwezo wa maghala kuhifadhi nafaka kati ya tani 700,000 na milioni moja ifikapo juni, 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Amesema mpango huo unakwenda sambamba na utekelezaji wa malengo malengo ya kuzitanua zaidi shughuli za wakala ikiwemo kuimarisha na kuongeza vituo vya ununuzi nchi nzima
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana mkurugenzi huyo amesema NFRA imebadili mtazamo wake wa awali kutoka kuwa taasisi ya kuhifadhi nafaka tu na badala yake kuwa ni taasisi inayonunua na kuuza nafaka ndani na nje ya nchi.
“Mpango huu umekuja kutokana na uhitaji wa mazao ya nafaka hasa katika nchi Jirani na maeneo mbalimbali duniani. Kama taasisi tumelazimika kujipanga na kutumia fursa ya ukuaji wa soko,” alisema.
Kwa mwaka huu, NFRA imeingia mikataba na nchi za Jamhuri ya Congo (DRC) na Zambia wa kuuza tani 1,150,000 za mahindi.
Kati ya tani hizo, Zambia imenunua tani 650,000 za Mahindi na sehemu ya nafaka hiyo imeshaanza kusafirishwa ambapo Jamhuri ya Kongo (DRC Cong) imenunua tani 500,000 zitakazosafirishwa kwenda katika jimbo la Katanga.
“Kwetu sisi hii ni fursa kubwa na itawasaidia wakulima wetu na wafanyabiashara kuongeza mapato yake lakini sambamba na kukuza uchumi wa nchi kwa kuingiza fedha za kigeni,” aliongeza Dk. Komba.
Alisema biashara itaongezeka zaidi baada ya kupata hifadhi ya kutosha ya nafaka kwa usalama wa nchi yetu pamoja nafaka za ziada tunauzwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Amesema uhitaji wa chakula ni mkubwa na ndiyo maana kama taasisi imeamua kujiongeza na kuja wa mtazamo wa kufanya biashara badala ya kuhifadhi nafaka ghalani.
“Kama NFRA tuna mipango ya kununua tani 600,000 kutoka kwa wakulima katika utaratibu wake wa kuhifadhi nafaka.
ZINAZOFANANA
Polisi: Waharifu 2024 wapungua mkoani Songwe
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Mil.600 zatengwa kupeleka umeme Kijiji cha Ijinga – Magu