December 3, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mshukiwa wa mauaji wanawake 42 atoroka mahabusu

 

RAIA wa Kenya aliyekiri kuhusika na mauaji ya wanawake 42 ambao baadhi yao miili yao ilipatikana ikiwa imetupwa kwenye dampo la Kware jijini Nairobi, ametoroka gerezani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Nairobi, Adamson Bungei mshukiwa huyo Collins Jumaisi (33) pamoja na wafungwa wengine 13 wametoroka katika Kituo cha Polisi cha Gigir.

Jumaisi alikamatwa na polisi mwezi uliopita baada ya miili ya wanawake waliokatakatwa vipande kupatikana ikiwa imetupwa kwenye eneo la taka katika mtaa wa Embakasi, nje kidogo na jiji la Nairobi.

Kwa mujibu Bungei, mshukiwa huyo na wafungwa wenzie 13 walitoroka gerezani usiku wa kuamkia leo Jumanne.

Miongoni mwa wafungwa waliotoroka gerezani ni pamoja na raia 13 wa Eriteria kulingana na taarifa ya msemaji wa polisi.

Jumaisi alifikishwa mahakamani Ijumaa ya wiki iliopita ambapo hakimu aliagiza azuiliwe kwa muda wa miezi 30 zaidi kutoa nafasi ya uchunguzi kukamilika.

Miili 10 ya wanawake waliokuwa wamekatwakatwa ilipatikana ikiwa imefungwa kwenye mifuko ya plastiki na kutupwa kwenye eneo la taka katika mtaa wa Kware.

Jumaisi alikamatwa tarehe 15 ya mwezi Julai karibu na eneo la burudani ambapo alikuwa akifuatilia michezo ya Euro 2024.

About The Author

error: Content is protected !!