December 27, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Waandamanaji wamteua rais wa muda Bangladesh

 

MSHINDI wa Tuzo ya Nobel anayejulikana kama “benki kwa maskini” atalenga kuleta utulivu nchini Bangladesh baada ya kuitikia wito wa waandamanaji wanafunzi kumtaka aongoze kwa muda nchi hiyo yenye machafuko kufuatia wiki kadhaa za maandamano mabaya dhidi ya serikali. DHAKA, Bangladesh

Muhammad Yunus, 84, ataongoza serikali ya mpito kufuatia kupinduliwa kwa waziri mkuu wa nchi hiyo ya Asia Kusini Sheikh Hasina na kuvunjwa kwa Bunge, aneeleza katibu wa vyombo vya habari wa rais wa Bangladesh.

Yunus ni mjasiriamali wa kijamii na mtaalamu wa masuala ya benki ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2006 kwa kazi yake ndogo ya ufadhili ambayo ilisaidia kupunguza umaskini nchini Bangladesh na ilikubaliwa kote ulimwenguni.

Sheikh Hasina, ambaye Januari 7, 2024 alishinda muhula wake wa tano, amekimbília uhamishoni India baada ya maandamano makubwa ya mwezi mmoja dhidi ya serikali yake.

About The Author

error: Content is protected !!