October 13, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dodoma watembelea miradi ya gesi asilia kwa teknolojia ya uhalisia pepe

MAONYESHO ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yamekuwa ni sehemu ya wananchi kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya nishati ikiwemo miradi ya gesi asilia na mafuta. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Katika Banda la Wizara ya Nishati wananchi wameonesha kuvutiwa na teknolojia ya uhalisia pepe (Virtual reality) ambayo inawawezesha wananchi kuona moja kwa moja miradi ya uzalishaji, uchakataji na usambazaji wa gesi asilia iliyopo mkoani Mtwara na Lindi.

Kupitia teknolojia hiyo wananchi wameona namna gesi inavyozalishwa kutoka kwenye visima na kuingizwa kwenye mitambo ya uchakataji kisha kusafirishwa kwa bomba kwenda kwenye matumizi mbalimbali ya viwandani, kuzalisha umeme, kwenye magari, taasisi pamoja na matumizi ya majumbani.

Aidha, Wizara ya Nishati inaendelea kutoa elimu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).

About The Author