Benki ya Biashara Tanzania (TCB) leo Ijumaa imesaini mkataba wa makubaliano (MOU) ya kimkakati na Wakala wa Serikali wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar ( ZEEA) kwa lengo la kuanzisha mpango maalum wa mikopo utakaonufaisha makundi maalum wakiwemo wanawake na vijana wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Mpango huo pia unakusudia kuchochea ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo jijini Dar es salaam, Katibu mkuu ofisi ya Rais kazi uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mariam amesema tayari Sh bilioni mbili zimeshakusanywa na halmashauri visiwani humo ili kuanza uwezeshaji huku akiitaka Benki ya TCB kuhakikisha inafanya tathmini ya mikopo wanayotoa kwa makundi hayo ili ziweze kurejeshwa kwa wakati na wengine waweze kukopa.
Ameeleza kuwa mpango huo wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao.
“Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha
uchumi wa ndani, kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na ukosefu wa ajira na kuleta maendeleo na kuwa kupata fursa ya mikopo jambo ambalo ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa biashara
ndogondogo na za kati.
Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TCB, Adam Mihayo amesema mkataba huo wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla na kwamba unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.
Amesema mkataba huo utawezesha kutoa mikopo nafuu ya kiasi cha Sh milioni 30 kwa kila kikundi, huku wakipewa muda miezi 24 sawa na miaka miwili kwa kutoa mikopo nafuu kwa makundi hayo.
Ameongeza TCB na ZEEA watawasaidia wajasiriamali kupanua biashara zao, kutengeneza fursa mpya za ajira, na hivyo kupunguza uhaba wa ajira.
“Mpango huu pia utazisaidia biashara kujiendesha, kukabiliana na mfumuko wa bei, pamoja na kuwekeza katika vitendea kazi, na kuzipa ustahimilivu, tuna furaha kushirikiana na ZEEA kuwainua wajasiriamali wanawake, vijana na makundi mengine maalum yaliyomo visiwani Zanzibar,” alisema Mihayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA, Juma Burhan Mohamed amesema wanalenga kuipatia benki ya TCB kiasi cha Sh bilioni 1.8 ili waanze utoaji wa mikopo hiyo na kwamba mpango huu unaendana na lengo la kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa kujenga uchumi jumuishi kwa
kuhakikisha makundi maalum yanaziinua biashara binafsi, pamoja na kuimarisha mfumo mzima wa uchumi na kutengeneza mazingira imara ya kiuchumi.” alisema
Pia yanakusudia kuimarisha uchumi wa buluu visiwani Zanzibar.
Amesema mpango huo wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao.
ZINAZOFANANA
Rich Panda kukupandisha kwenye mkwanja
Vodacom yazindua Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kupeleka huduma mtaani
5 Hot Strike mchezo wa kasino rahisi kucheza na kushinda