September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kamala Harris achangiwa bilioni 534 za kampeni

 

MAKAMU wa rais nchini Marekani na mgombeaji wa kiti cha urais, Kamala Harris amechangiwa Dola za Marekani 200 milioni (Sh 534.1 bilioni) za kufanya kampeni. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Hatua hiyo imejiri baada ya Rais wa taifa hilo, Joe Biden kutangaza kuacha kuwania urais dhidi ya mpinzani wake anayepeperusha bendera kwa tiketi ya Republican, Rais mstaafu, Donald Trump.

Biden alimpisha Kamala kuwa mgombea atakapeperusha bendera ya kuwania urais kupitia chama cha Democratic.

Mkurugenzi wa mawasiliano kitengo cha kampeni, Michael Tyler amesema kiwango hicho ni kwa mujibu wa kamati ya kuongoza kampeni ya Kamala ambayo ilitangaza jumla ya pesa zilizokusanya za kampeni kufikia jana Jumapili.

Aidha, kamati hiyo iliongeza kwamba kati ya pesa hizo zilizokusanywa, asilimia 66 ya waliochanga ni wahisani waliojitolea kuchanga peza za kampeni kwa mara ya kwanza katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2024.

Aidha, zaidi ya wahisani 170,000 wamejitolea bila malipo kumsaidia Kamala katika shughuli za kumpigia debe.

“Kasi alionayo pamoja na nguvu ni ishara tosha kwamba Kamala amejituma kuwania urais. Ni kinyang’anyiro kitakachokuwa kikiamuliwa na idadi ndogo ya kura kutoka katika maeneo machache tu,” alisema.

Kwa upande mwingine, kitengo cha mawasiliano cha Trump kiliambia waandishi wa habari kwamba mapema mwezi Julai mwaka huu, kilikuwa kimechanga dola za Marekani 331 milioni katika kipindi cha miezi mitatu, na kupiku Biden aliyekusanya dola 264 milioni.

Pesa hizo zilikuwa zimechangishwa katika kampeni ya rais Biden na wanachama wa mrengo wake wa chama cha Democratic katika muda sawa wa miezi mitatu.

Aliyekuwa spika katika bunge la Amerika, Nancy Pelosi, Kiongozi wa walio wengi katika bunge la Seneti, Chuck Schumer, Kiongozi wa wengi, Hakeem Jeffries, kiongozi wa walio wachache Jim Clyburn, aliyekuwa rais wa Amerika Bill Clinton na aliyekuwa katibu katika ikulu ya rais Hillary Clinton ni miongoni mwa viongozi waliotangaza kumuunga mkono Kamala.

About The Author