April 8, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Israel yadai kumuua mkuu wa intelijensia wa Iran

Spread the love

WAZIRI wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema Jumatatu kuwa jeshi la nchi hiyo limemuua mkuu wa intelijensia wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran.Anaripoti Mwandishi wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika taarifa rasmi, Katz alisema hatua hiyo ni sehemu ya operesheni pana dhidi ya viongozi wa kijeshi wa Iran. “Walinzi wa Mapinduzi wanawashambulia raia na sisi tunawaondoa viongozi wa ugaidi,” alisema. “Viongozi wa Iran wanaishi kwa hofu ya kulengwa.

Tutaendelea kuwawinda mmoja baada ya mwingine.”

Hata hivyo, hakutoa maelezo ya kina kuhusu operesheni hiyo wala kuthibitisha utambulisho wa aliyedaiwa kuuawa.

Katika kauli yake, Katz pia alidai kuwa Israel imeharibu kwa kiasi kikubwa sekta za chuma na petrokemikali za Iran, akisema mashambulizi hayo yanalenga kudhoofisha uwezo wa kiuchumi na kijeshi wa taifa hilo.

“Tutaendelea kusambaratisha miundombinu ya taifa la Iran na kusababisha kudhoofika na hatimaye kuporomoka kwa utawala huo, pamoja na uwezo wake wa kuendeleza mashambulizi dhidi ya Israel,” alisema.

About The Author

error: Content is protected !!