Benjamin Netanyahu
BENJAMIN Netanyahu, Waziri Mkuu wa muda mrefu nchini Israel, ametaka mataifa mengine ulimwenguni, kujiunga katika vyake na Iran. Amesema, mashambulizi ya Iran ya majuzi dhidi ya taifa lake na mataifa ya Ghuba, ni kitisho kwa dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Netanyahu amesema, Iran inatishia usalama wa dunia, na kwamba mashambulizi hayo yanaonesha taifa hilo, kuwa kitisho kwa ulimwengu mzima.
“Iran siyo kitisho kwa Mashariki ya Kati pekee, kwa dunia nzima,” alisema na kuongeza, “Iran sasa ina uwezo wa kushambulia hadi barani Ulaya.
Haya yanajiri wiki tatu baada ya Netanyahu na swahiba wake, Donald Trump, rais wa Marekani, kuanzisha vita dhidi ya serikali ya Kizayuni ya Iran.
Netanyahu alikuwa akizungumzia kombora lililorushwa na Jamhuri hiyo ya kiislamu kusini mwa nchi yake, lililoleta maafa makubwa na jingine lililolenga kambi za pamoja za kijeshi za Marekani na Uingereza katika eneo la Diego Garcia katika bahari Hindi, kilomita 4000 kutoka Iran.
Aidha, Netanyahu ameishutumu Iran kwa kutaka kuvuruga njia za biashara za dunia kwa kutaka kushambulia meli zozote zitakazopita katika mlango bahari wa Hormuz.
Netanyahu ametumia miongo kadhaa kujiandaa kwa makabiliano haya na Iran, na maisha yake ya kisiasa yamejengwa juu ya ahadi ya kuilinda Israel dhidi ya adui wake – Iran.
Baada ya kuanzisha vita vya moja kwa moja dhidi ya utawala wa Iran pamoja na mshirika wake Marekani, kauli za Netanyahu kuhusu vita hivyo hazijawa na ufasaha, anaelezea kuwa mashambulizi hayo ni “kampeni ya uwepo wetu wenyewe.”
Mkuu wa majeshi ya Israel ameelezea mashambulizi hayo kama “operesheni ya kulinda maisha ya baadaye katika ardhi ya mababu zetu kwa vizazi vijavyo.”
Mmoja wa washauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Netanyahu amesema, “hii ni fursa ya kipekee ya kubadilisha mwelekeo wa Mashariki ya Kati.”
“Hiki ni kilele cha kile ambacho Netanyahu amejaribu kukipa jina jipya kama ‘Vita vya Ukombozi,’ ambavyo kwa mtazamo wake vilianza tarehe 7 Oktoba 2023. Na hii kama si vita vya mwisho, basi vita kubwa dhidi ya Iran,” anaeleza Neri Zilber, mwandishi wa habari wa Tel Aviv na mshauri wa kisiasa wa Israel Policy Forum, taasisi ya utafiti ya Marekani.
Katika vita vya mwaka uliopita dhidi ya Iran, Waziri mkuu wa Israel alitangaza “ushindi wa kihistoria” ambao utadumu hadi vizazi vijavyo na kwamba ameondoa vitisho viwili vya kimsingi hasa silaha za nyuklia na makombora yake ya masafa marefu.
Miezi minane baadaye, Israel ilirudi tena vitani, Netanyahu akidai Iran ilikuwa ikijenga upya na kwa kasi mpango wake wa makombora na ilikuwa inapanga kuuhamishia, pamoja na mpango wake wa nyuklia, chini ya ardhi.
ZINAZOFANANA
Polisi ahukumiwa miaka miwili jela kwa kusababisha kifo
Iran yathibitisha kuwa Waziri wa Ujasusi ameuawa
Radi yaua wanafunzi watatu Dar