Mhuli Ngeleja
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, Mhuli Ngeleja amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 20 Machi 2026 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi, na kueleza kuwa chama kimepoteza kiongozi shupavu, mwadilifu na aliyejitolea kwa dhati kukitumikia chama na wananchi.
“Tumejawa na huzuni kuu kwa kupoteza nguzo muhimu ndani ya chama, aliyejipambanua kwa uchapakazi na uzalendo wa hali ya juu,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa marehemu Ngeleja alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha umoja wa wanachama, pamoja na kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed, amesema kuwa chama kipo katika maandalizi ya taratibu za mazishi huku akiahidi kutoa taarifa kamili baadaye.
ZINAZOFANANA
Magufuli alibadilisha fikra za uongozi Tanzania – Dk. Nchimbi
Balozi Nchimbi kuongoza miaka mitano ya kifo cha Magufuli
Mahakama yaamuru Wakazi kumlipa Mil 100 Baba Levo