MKURUGENZI wa Sheria na haki za binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wakili Gaston Galubindi, amesema kuwa kitendo cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kukimbilia Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya uhaini inayomkabuli Tundu Lissu, Mwenyekiti wa chama hicho, hakikubaliki kwenye msimamo wa kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Wakili Galubindi amekitaja kitendo hicho kwani sheria imeelekeza wazi kuwa hakuna rufani kwenye uamuzi wa maombi madogo kwenye mashauri ya msingi, kwa kuwa kitendo hicho sawa na kupaki basi na kuwaona kuwa waendasha mashtaka kwenye kesi hiyo wameshindwa kuendelea na shauri hilo “kwa kuwa hawana hoja ya kuendelea na hii kesi wameamua kupaki basi wakitaka Lissu aendelee kuteseka gerezani”
“Mahakama ya Rufani haiwezi kufanya marejeo hayo hivyo wanakwenda kuipaki kesi hiyo kwa lengo la kutaka kuendelea kumkomoa Mwenyekiti wetu.”
Wakili huyo aliyezungumza na MwanaHALISI Digital kwa njia ya simu amesema kuwa msimamo wa chama hicho ni kwamba wanafahamu kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa yenye lengo la kuwaziba midomo wapinzani lakini wao hawatanyamaza .
“Tutaendelea kupaza sauti nje na ndani ya nchi kueleza juu ya haya yanayoendelea ambayo hayakubaliki kisheria na wala Katiba,” amesema Wakili Galubindi.
Akinukuu Katiba ya nchi ibara 59 (B) (4) katika kutekeleza mamlaka yake Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa huru hataingiliwa na mtu au mamlaka yoyote na atazingatia nia ya kutenda haki, matumizi mabaya ya utaritibu wa utoaji haki, kwa hiyo ni matumizi mabaya ya utaribu wa utoaji haki”
Amesema kuwa DPP kufungua shauri ambalo halina maslahi na umma na kwamba wanaendesha shauri hilo wakijua halina maslahi kwa taifa.
ZINAZOFANANA
Polisi ahukumiwa miaka miwili jela kwa kusababisha kifo
Iran yathibitisha kuwa Waziri wa Ujasusi ameuawa
Radi yaua wanafunzi watatu Dar