November 23, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

CP Kaganda atoa uzoefu Polisi Jamii Marekani, washiriki waipokea mbinu hiyo

 

KAMISHINA wa Polisi Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Suzan Kaganda ametoa uzoefu wa masuala ya Polisi Jamii yanavyosaidia kulinda amani katika maeneo yanayofanyika bila jeshi la Polisi kuwepo. Anaripoti Abel Paul, Chicago Marekani … (endelea).

CP Kaganda ametoa uzoefu huo katika mafunzo kwa askari wa kike na wasimamizi wa sheria duniani yanayoendelea jijini Chicago, Marekani.

Uzoefu huo umetolewa mbele ya maelefu waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yaliyohusisha nchi zaidi ya 64 ambapo ametoa uzoefu wake katika masuala ya Polisi Jamii na namna ambavyo wananchi wanaweza kushiriki kulinda amani ya eneo husika bila ya kuwa na Jeshi la Polisi wala Jeshi lolote katika eneo lenye changamoto ya amani.

Aidha ameongeza kuwa suala la amani ni jambo ambalo linatakiwa kushirikisha Jamii ili amani na utulivu wa eneo husika kuimarika kutokana na ushiriki kamili wa wananchi katika ulinzi wa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi akiweka wazi kuwa suala la amani ya eneo husika linatakiwa kuanza na Jamii husika.

Sambamba na hilo, CP Kaganda akasisitiza kuwa suala la Polisi jamii ni njia nzuri katika masuala ya ulinzi wa amani kutoka na tafiti alizozifanya na uzoefu wake akiwa Mkuu wa operesheni za kulinda amani katika eneo Abyei Sudan Kusini.

Mbali na hilo washiriki wengine kutoka nchini Tanzania wakaeleza namna mafunzo hayo yalivyowaimarisha katika kujiamini kiutendaji na nafasi wanazopewa hudumu huku waki weka wazi kuwa pindi watakaporudi nchini wategemee mabadiliko makubwa kutokana mafunzo hayo.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi, SACP Johari Saidi yeye akaeleza namna mafunzo hayo yalivyowapa mwanga katika mgawanyo wa majukumu bila kuathiri familia walizonazo ikiwa ni pamoja na namna bora ya utunzaji wa afya kwa askari kutokana na unyeti wa majukum makubwa waliyonayovyombo vya ulinzi.

About The Author