Tundu Lissu akiwa mahakamani
MAHAKAMA Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imeendelea kusikiliza shauri Na.19605/2025 la uhaini Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo Lissu amehitimisha kumuuliza maswali ya dodoso shahidi wa 14 sasa anamsubiri shahidi wa 15. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Shauri hilo linalosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dustan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.
Lissu: Waambie majaji kama tutafanya vurugu na kuuvuruga uchaguzi huo kama yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi P9: Hayapo
Lissu: Uliendelea kusema, alisema lazima tukichafue, kweli si kweli?
Shahidi P9: Kweli.
Lissu: Hayo maneno yapo au hapo?
Shahidi P9: Sasa mbona unarudia maswali. “Hayapo,”.
Lissu: Twende kwa yaliyotokea 22 Aprili 2025, ulisema siku hiyo ulipigiwa simu na polisi kwenda kituo cha polisi Mwanjelwa?
Shahidi P9: Kweli.
Lissu: Sasa soma pale palipoanzia na leo tarehe 22 Aprili 2025, mpaka nitakapokwambia basi?
Shahidi P9: Anasoma…
Lissu: Kwenye hiyo sehemu kuna sehemu kumeandikwa kituo cha polisi Mwanjelwa?
Shahidi P9: Kweli haijaandikwa.
Lissu: Na ukasema ulipofika walisema wanataka kukuhoji tena kwa matukio yaliyokuleta hapa?
Shahidi wa P9: Kweli.
Lissu: Waambie kama hayo maneno yapo kwa tukio lililokuleta hapa?
Shahidi P9: Hayapo.
Lissu: Kwenye ushahidi wako jana, ulisema nilihojiwa na mtu mmoja na mwingine alichangia kwa kuniuliza maswali mbalimbali, waeleze majaji kama hayo maneno yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa P9: Hayapo.
Lissu: Ukasema kuwa “Niliona clip ya Tundu Lissu ….,” waeleze hayo maneno kama yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa P9: Hayapo.
Lissu: Sijamalizana na wewe, nataka ukitoka hapa ukawaeleze mapolisi kwamba kule hakufai!
Lissu: Ulisema mimi kama mwananchama wa Chadema, nilishawishika na kwamba nitafanya uasi, hayo maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa P9: Yapo.
Lissu: Sasa nataka uwaambie majaji kwamba wewe ni mwanachama wa Chadema au sio?
Shahidi wa P9: Mimi sio mwanachama wa Chadema.
Lissu: Kwenye maelezo yako na ushahidi wako wa jana, ulisema mwaka 2024 ulivutiwa na sera na kuamua kuwa mwanachama wa Chadema, kweli au sio kweli?
Shahidi wa P9: Kweli.
Lissu: Waambie majaji, wafuasi wa Chadema huwa wanaandikishwa wapi?
Shahidi wa P9: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama wafuasi huwa wanatambulishwa wapi?
Shahidi wa P9: Sijui.
Lissu: Waeleze kama huwa wanaalama usoni?
Shahidi wa P9: Hapana.
Lissu: Na ulisema baada ya kuwa mfuasi ulishiriki katika matembezi ya amani, kweli au sio kweli?
Shahidi wa P9: Kweli.
Lissu: Waambie waheshimiwa kama ulijiandikisha sehemu yoyote?
Shahidi wa P9: Hapana.
Lissu: Sasa shahidi hukuwahi kujiandikisha popote, huna alama yoyote kuwa ni mfuasi wa Chadema, waeleze majaji wataamini vipi kwamba wewe ni mfuasi wa Chadema?
Shahidi wa P9: Mimi sijui hilo ni suala la amani.
Lissu: Unasema tulihamasishwa kushiriki kongamano la vijana lililopangwa kufanyika Mbeya, waambie kama uliwahi kupewa mualiko wowote hata wa simu?
Shahidi wa P9: Hapana sikupewa mualiko wowote.
Lissu: Kama kiongozi wa chama aliwahi kukufata ili kukupa taarifa ya kongamano?
Shahidi wa P9: Hawakunifata.
Lissu: Kama hawakukufata inamaana hawakujui?
Shahidi wa P9: Sio lazima wanijue wote.
Lissu: Kwa maelezo yako ya ushahidi ya jana, umesema ulisoma Veta Mbeya kati ya 2008-2010 ulipohitimu, kweli au sio kweli?
Shahidi wa P9: Kweli.
Lissu: Waeleze majaji kama umewasilisha cheti cha kuhitimu?
Shahidi wa P9: Sijawasilisha kwasababu hakina umuhimu.
Lissu: Wataaminije, Kwasababu maneno matupu hayavunji mfupa, umesajiliwa kama fundi umeme wa majumbani na viwandani?
Shahidi wa P9: Ndio nimesjiliwa.
Lissu: Waeleze majaji kama umeleta hati ya kusajiliwa?
Shahidi wa P9: Hapana.
Lissu: Shahidi umesema tarehe 4 aprili 2024, ukiwa na jamaa zako nyumbani kwako, “tukawa tunajadili kauli ya mwenyekiti kwamba tukichafue, ni kweli au si kweli?
Shahidi wa P9: Ni kweli.
Lissu: Umewataja hao jamaa zako wakati unatoa ushahidi?
Shahidi wa P9: Hapana.
Lissu: Wakati tunazungumza jamaa yangu akaniomba namba yangu ya simu, jamaa ambaye simfahamu, unakumbuka hayo maneno?
Shahidi wa P9: Ndio nakumbuka.
Lissu: Inawezekana mtu usiyemfahamu kuwa jamaa yako, hiyo inaingia akilini?
Shahidi P9: Inawezekana.
Lissu: Na jamaa yako ambaye humfahamu akakuomba namba yako ya simu na ukampatia? Inaingia akilini?
Shahidi wa P9: Ndio inaingia akilini.
Lissu: Ndivyo ulivyofundishwa na mapolisi.
Lissu: Kwa vile unafanya kazi ya fundi umeme kwa malipo, una leseni ya biashara?
Shahidi wa P9: Sina leseni ya biashara kwasababu sina ofisi
Lissu: Una TIN namba ?
Shahidi wa P9: Ndio.
Lissu: Umeionyesha?
Shahidi wa P9: Hapana kwasababu haijahitajika.
Lissu: Tarehe 5 Aprili siku ambayo unakamatwa, unasema ulipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mteja, na ukasema tulipoonana akajitambulisha kuwa ni afisa wa polisi na akanionyesha kitambulisho chake, waambie waheshimiwa majaji kama unakumbuka jina la hicho kitambulisho?
Shahidi wa P9: Nakumbuka ni Vicent.
Lissu: Waeleze majaji kama hilo jina lipo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa P9: Halipo.
Lissu: Hiyo tarehe 5 April uliandika maelezo kweli au si kweli?
Shahidi wa P9: Kweli.
Lissu: Na maelezo ya siku hiyo yalihusu uchochezi na kuzuia uchaguzi, kweli au si kweli?
Shahidi wa P9: Kweli
Lissu: Waambie majaji hiyo tuhuma ya uchochezi na kuzuia uchaguzi imeishia wapi?
Shahidi wa P9: Sijui.
Lissu: Waeleze majaji tangu tarehe 5 april 2024 umepelekwa Mahakamani kwa tuhuma hizo?
Shahidi wa P9: Sijawahi kupelekwa.
Lissu: Waeleze majaji ulipoitwa polisi kwa mara ya pili 22 april 2025 kama ulielezwa tuhuma za uchochezi na kuzuia uchaguzi?
Shahidi P9: Ndio nilielezwa.
Lissu: Angalia maelezo yako shahidi halafu tuonyeshe wapi uliuzwa juu ya tuhuma hizo?
Shahidi wa P9: Mimi nilieleza lakini wao hawakuandika.
Lissu: Imekula kwako kwasababu wanasema haya ni maelezo yako. Wewe ni shahidi kwenye kesi dhidi yangu, kweli si kweli.?
Shahidi wa P9: Kweli.
Lissu: Na ndio maana umekuja kutoa ushahhidi jana na leo, kweli si kweli?
Shahidi wa P9: Kweli.
Lissu: Nikisema walikukamata tu ili uje kutia ushahidi dhidi yangu nitakua nakosea?
Shahidi wa P9: Mimi sifahamu.
Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama unajua kuwa hakuna kosa la kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa P9: Ni kosa.
Lissu: Waambie majaji ni kwa mujibu wa sheria gani?
Shahidi wa P9: Nimi sio mwanasheria.
Lissu: Ni sheria gani.
Shahidi wa P9: Mimi najua kuzuia uchaguz kwa njia ya vurugu ni kosa lakini sheria gani sijui
Lissu: Kama hujui sema sijui, sio kuleta ujuaji tu. Lissu: Kwani mimi nimeshatakiwa kwa kosa la vurugu?
Shahidi wa P9: Umeshtakiwa kwa uhaini.
Lissu: Shahidi ulikujaje Dar es Salaam?
Shahidi P9: Nilipanda basi.
Lissu: Nani alikwambia uje kutoa ushahidi?
Shahidi wa P9: Nililetewa wito.
Lissu: Nani alikuletea?
Shahidi wa P9: Aliniletea mwenyekiti wa serikali za mtaa.
Lissu: Anaitwa nani?
Shahidi wa P9: Siwezi kukutajia kwasababu za kiusalama.
Wakili wa Serikali Nassoro Katuga: Sisi tunapinga hilo swali kwasababu za kiusalama. Kwa hiyo tunaomba hilo swali asiulizwe.
Lissu: Waheshimiwa majaji hilo pingamizi la wakili la Serikali halina maana yoyote, kwasababu shahidi mwenyewe amesema kwamba alipelekewa summons (wito) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti ni ofisa wa serikali, lakini vilevile Mahakama haitaweza kujua kama huyu shahidi ni mkweli au ni muongo kwahiyo swali langu ni halali na ninaomba pingamizi lao litupitiliwe mbali, lakini huyo Mwenyekiti sio mtu ambaye amelindwa na sheria.
Katuga: Sisi tunaomba swali hilo shahidi asiulizwa kwasababu swali hilo litapelekea utambuzi wa shahidi huyu na kama tunavyojua humu ndani kuna wafuasi wake, researchers wake wanaweza wakaenda kumtafuta ili kumtambua shahidi huyu.
Lissu: Naomba ondoa hiyo kauli yako mimi sijazungumzia kuhusu wafuasi wangu humu.
Katuga: Naondoa hiyo ilikua ni by the way lakini msimamo wetu ni kwamba swali hilo shahidi asiulizwe.
Jaji: Tuendelee na cross examination (dodoso) bila hilo jina.
Lissu: Lakini waheshimiwa majaji mnaweza kuona namna cross examination yangu inavyokua limited (inamipaka) lakini naomba niendelee.
Lissu: Shahidi umekujaje hapa?
Shahidi P9: Nimependa basi.
Lissu: Nani amekulipia nauli?
Shahidi P9: Nimejilipia mwenyewe.
Lissu: Umefikia wapi?
Shahidi wa P9: Kwa ndugu yangu.
Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama kuna kiongozi au mfuasi anajua kama unakuja kutoa ushahidi?
Shahidi P9: Ndio wapo baadhi.
Lissu: Waliwahi kukutishia?
Shahidi wa P9: Ndio.
Lissu: Unajua hilo ni kosa.
Shahidi wa P9: Hilo ni kosa la jinai
Lissu: Umewataja?
Shahidi wa P9: Siwezi kuwataja kwa usalama.
Lissu: Waeleze majaji kama ulitoa taarifa kituo cha polis
Shahidi wa P9: Ndio.
Lissu: Kituo cha polisi kipi?
Shahidi P9: Sasa nikitoa taarifa hiyo hapa si itakua navunja usalama?
Lissu: Hebu jibu swali bwana tusisumbuane?
Mahakama: Shahidi hebu jibu hilo swali
Shahidi P9: Nilitoa kituo cha polisi Ilomba.
Lissu: Ulipewa RB?
Shahidi wa P9: Ndio
Lissu: umeitoa hapa mahakamani?
Shahidi wa P9: Hapana
Lissu: Polisi walichukua hatua gani?
Shahidi P9: Walisema watafatilia.
Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama kuna mtu yoyote amekamatwa?
Shahidi wa P9: Hapana.
Lissu: Waambie kama kuna mtu yoyote amepelekwa mahakamani:
Shahidi wa P9: Hakuna.
Lissu: Waheshimiwa majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Wakili wa Serikali: Leo tunashahidi mmoja, tunaomba mapumziko kidogo halafu tuje na shahidi mmoja aliyebaki, kwasababu jana hatukupumzika.
Jaji: Mshitakiwa unasemaje?
Lissu: Tukienda kwa utaratibu huu tutachukua mida mrefu sana, Mahakama ilisema upande wa serikali ulete mashahidi wasiopungua watatu, kwanin hawajaleta hao mashahidi wengine. Upande wa mashtaka wanatakiwa wawe na mshahidi wengine kama walivyotakiwa na mahakama.
Katuga: Jana tulisema tutakuja na shahidi mmoja then twende kwenye kuwasilisha hoja za application yetu, hatujaweza kuja na mashahidi wengi ili tupate muda wa kutosha kwasababu yeye alisema ana-objection.
Mahakama inakwenda kwenye mapunziko mafupi, indelea kufuatilia MwanaHALISI itaendelea…
ZINAZOFANANA
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yaridhishwa na uzalishaji umeme
Aliyemkamata mhamasishaji vurugu Mbeya atoa ushahidi kesi ya Lissu
Kardinali Pengo kuzikwa Pugu Feb 28