February 19, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi ya Lissu: Shahidi aeleza alivyomkamata aliyehamasisha vurugu za uchaguzi

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

SHAHIDI wa 12 kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameeanza kutoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Ni Ofisa wa upelelezi aliyejitambulisha kwa jina la H.1937 D. Vicent anayefanya kazi Mbeya aliyejiunga na Jeshi la Polisi mwaka 2012.

Akitoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.

Ofisa huyo mwenye miaka sita kwenye upelelezi alieleza mahakama kuwa majukumu yake ni kupeleleza kesi, kukamata na kutoa ushahidi.

Amedai tarehe 5 April 2025, akiwa kazini anadai alipokea maelekezo ya kumkamata ‘P8’ aliyekuwa anahamasisha kwenye vijiwe mbalimbali kuchochea uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike “Kwa hiyo nikapewa maelekezo ya kumkamata”.

Anadai kuwa alipewa namba ya simu ya huyu mtuhumiwa na Mkuu wake wa Kituo alizozipata kupitia msiri wake aliyetoa taarifa hizo.

Ameieleza kuwa alipobaini kuwa mtu huyo (P8) ni fundi umeme alijifanya mteja anayetaka huduma yake .”Niliwasiliana naye kirafiki kama mteja na kukubaliana tuonane maeneo ya Kabwe kweli tulikutana hapo Kabwe, na nilivyokutana naye nikamueleza kwamba mimi shida yangu sio umeme nikajitambulisha kama mimi ni polisi nikamuonesha kitambulisho”.

Ameieleza mahakama kuwa alimueleza P8 kwamba amekwenda kumkamata kwa kuwa anatuhumiwa kwa uchochezi na kuhamasisha vurugu na kuzuia uchaguzi.

Anadai P8 naye alikuwa muelewa na hakuwa na vurugu hivyo walioongozana mpaka katika kituo cha polisi.

Ameieleza mahakama hiyo kuwa baada ya kumkabidhisha kwenye kituo cha Polisi yeye aliendelea na majukumu mengine.

About The Author

error: Content is protected !!