February 12, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama: Kumnyima chakula Lissu ni kukiuka haki za binadamu

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

MAHAKAMA Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imesema kuwa kitendo cha maofisa wa magereza kumnyima chakula Tundu Lissu anayeshtakiwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za uhaini kimeikuka haki za binadamu. Anaripoti Fedrick Gama, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yasemwa leo tarehe 12 Februari 2026 na Jaji Dunstan Ndunguru kiongozi wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza sahuri hilo akishirikiana na wenzake Jaji James Karayemaha, na Jaji Ferdinand Kiwonde, wakati mahakama hiyo ipo kwenye hatua za kutaka kumsikiliza shahidi wa tano baada ya shahidi wa nne kuhitimisha kutoa ushahidi wake.

Hayo yameibuka baada ya Lissu alieleza mahakama hiyo kuwa anakabiliwa na njaa. “Mheshimiwa. jaji sijala lakini naomba tuendelee tu ivyo ivyo maana ishu ya mimi kupewa chakula imeshindikana.”

Lissu ameongeza kuwa “magereza wamekataa kunipatia chakula, wamesema nitaenda kula gerezani.”

Jaji Ndunguru amesema kuwa chakula ni haki ya msingi kabisa na haitakuwa sahihi kuendelea na shauri hili bila mshitakiwa kupatiwa chakula.

“Wenzetu wa magereza mzingatie kuleta chakula, itakuwa ni kinyume cha haki za binadamu kumnyima mshitakiwa chakula,” alisema Jaji Ndunguru.

Shauri hilo limeahirishwa kesho saa 3 asubuhi.

About The Author

error: Content is protected !!