OTHMAN Masoud ‘OMO’ Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo amegoma kujiunga kwenye serikali ya umoja wa kitaifa (SUK), visiwani Zanzibar kama makamu wa kwanza wa Rais katika serikali hiyo, MwanaHALISI imeelezwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
OMO aliyemrithi Maalim Seif Sharifu Hamad aliyefariki tarehe 17 Februari mwaka 2021 alihudumu nafasi ya umakamu wa kwanza wa rais tangu tarehe 1 Machi 2021 baada ya chama cha ACT-Wazalendo kulipendekeza jina lake kisha Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kumteua kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.
OMO amedhihirisha mgomo huo kwenye vikao vya ndani ya chama hicho kwa kueleza msimamo wake waziwazi kuwa hawezi kujiunga kwenye serikali hiyo kwa kuwa haina dhamira ya kuikomboa Zanzibar .
Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa taifa hilo, alikuwa akipigania Zanzibar huru, Zanzibar moja yenye mamlaka kamili , Masoud anaamini kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM hakina dhamira ya kuifanya Zanzibar iwe na mamlaka kamili na kwa kuwa dhamira yake ilikuwa ni kuifanya nchi hiyo isimame kwa miguu yake imekwama kwa kile alichodai kuwa uchaguzi haukuwa wa haki.
Taarifa zinasema kuwa OMO hajakizuia chama chake kuingia kwenye serikali hiyo isipokuwa yeye hawezi ‘kutia ulimi wake puani’ hivyo chama hicho kipendekeze wanasiasa wengine waandamizi ndani ya chama hicho ili wajaze nafasi yake.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar chama kinachofuatia badala ya chama kilichoshika nafasi ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu kitaunda serikali kwa nafasi ya makamu wa kwanza wa rais na kutoa baadhi ya nafasi katika wizara kulingana uwiano wa asilimia za kura.
Katiba inatoa miezi mitatu kwa chama husika kujiunga serikali ya umoja huo tangu siku ambyo rais wa Zanzibar alipoapishwa ili shughuli za serikali ziendelee.
Chama hicho kimeanza kuchukua hatua za kuupinga uchaguzi huo ikiwa pamoja na kufungua shauri mahakama Kuu ya Zanzibar kupinga matokeo ya wawakilishi.
Chama cha ACT-Wazalendo kimeanza rasmi mchakato wa kisheria kudai haki za baadhi ya wawakilishi wake wanaodai kuporwa ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Kesi hizo zimeanza kutajwa asubuhi ya leo tarehe 10 Disemba 2025 katika Mahakama Kuu ya Zanzibar iliyopo Tunguu, katika hatua ambayo ACT-Wazalendo inaieleza kuwa ni sehemu ya mapambano yake ya kudai haki na kuleta uwazi katika mchakato wa uchaguzi.
Kwa mujibu wa kauli za viongozi wa chama hicho, uchaguzi wa mwaka 2025 uligubikwa na ubadhirifu na ukiukwaji wa taratibu, hasa katika maeneo ambayo chama kinadai kuwa kilishinda lakini matokeo yakabadilishwa kinyume cha sheria.
ACT-Wazalendo imeeleza kuwa itaendelea kufuata njia za kisheria ili kuhakikisha wawakilishi wanaodaiwa kuporwa ushindi wanarejeshewa haki yao.
ZINAZOFANANA
Siku ya Uhuru, isiyokuwa huru
Kesi kupinga uchaguzi Zbar zaanza
Desemba 9, kutoka kushuhudia gwaride hadi kubaki nyumbani