WANACHAMA wa klabu ya Simba wamebaki kwenye sintofahamu kufuatia mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu kufunga mkutano kiholela. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mkutano huo wa mwaka wa wanachama ulianza majira majira saa tatu asubuhi na kumalizika majira saa 6 uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Malalamiko ya wanachama hao yamekuja kufuatia kutopatiwa nafasi ya kuchangia na kupitisha kwenye baadhi ya ajenda zilizowasilishwa kwenye mkutano huo ikiweno ya marekebisho ya katiba.
Hali hiyo imewafanya wanachama hao kwa wingi wao ukumbini ambao walikaa kwa mafungu mafungu kutaka mweyekiti wa klabu hiyo kujiudhuru kwa kuwa wanaamini matatizo mengi ya klabu hiyo chanzo ni yeye.
ZINAZOFANANA
Rais wa FA ya Congo afungwa maisha jela
Je, Yanga kutetea taji la LIgi Kuu msimu huu?
ACT Wazalendo yawasilisha wasiwasi wa hali ya kisiasa UN