November 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mzimu wa Oktoba 29 unavyoitesa Serikali

 

NI siku 26 sasa tangu matukio ya tarehe 29 Oktoba yaliigubika Tanzania kiza cha moshi wa risasi zilizoacha simanzi na majonzi kwa wananchi. Bado mjadala wake hauzimi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kutokoma kwa mjadala huo unaweza kusema ni mzimu wa matukio hayo unaendelea kuitesa serikali.

Jaribu la kuhamisha mjadala huo umefeli. Kila propaganda inayoingizwa ndani yake linaibuka jipya linalohusu matukio yaleyale ya kuuawa kwa wananchi.

Leo tarehe 23 Novemba 2025 serikali kupitia msemaji wake imetoka hadharani kutema cheche kuvisakama vyombo vya habari vya nje hasa CNN kwa kudai kuwa havifanyi kazi kwa uweledi vinaripoti upande mmoja.

Wamesahau Shirika la Umma la Utangazaji (TBC) inalalamikiwa kuripoti habari za serikali na wadau wake na sio vinginevyo.

Kuundwa kwa tume ya umoja wa madola chini Rais wa zamani wa Malawi Dk. Lazarus Chakwera, Tume ya Rais Samia chini ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande.

Joto la matukio ya maandamano halipoi mbali za serikali kufungua kesi za uhaini kwa zaidi ya watu 140 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na baadaye Rais kumwagiza Mwendesha Mashtaka ya Umma ( DPP), kupembua wahalifu hao na kuwaweka kanda ya shauri hilo walioandamana kwa kufuata mkumbo.

Tarehe 15 Novemba 2025, Baraza la Maaskofu la Katoliki nchini (TEC), walitoa tamko la kutoa pole, kulaani mauaji na kusisitiza uchunguzi wa matukio hayo.

Siku zilizofuata yakaibuka makundi ya viongozi wa dini ya kiislam ambao walijikita zaidi kuijibu TEC na kudai kuwa baraza hilo limepotoka.

Haya yote yanadhihirisha kuwa 29 Oktoba haitafutika kirahisi.

About The Author

error: Content is protected !!