Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema akiwa mahakamani
TUNDU Lissu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye yupo katika gereza Kuu la Ukonga kama mshtakiwa wa tuhuma za uhaini katika mahakama kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam amesema kuwa atakuwa wa mwisho kutoka gerezani mpaka pale wafungwa wengine wote wa kisiasa watakapoachiwa. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu mwenye siku takribani 224 sawa na miezi saba gerezani anaamini kuwa mashtaka yake ni ya kisiasa na kwamba alishtakiwa ili uchaguzi Mkuu upite na kwamba haoni uhalali wa shauri hilo.
Lissu anadaiwa kusema kuwa yeye atakuwa wa mwisho kutoka gerezani mpaka pale wafungwa wote wa kisiasa watakaoachiwa .
Tarahe 17 Novemba aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alipochapicha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram picha iliyomuonesha akiwa ndani ya gari akaandika manano haya “ndio natoka kumtembelea Mwenyekiti wetu lissu gerezani kama alivyoniagaiza pale mahakamani juzi”
” Tumezungumza mambo mengi ya chama na nchi, yuko imara sana na amesema yuko tayari kuwa wa mwisho kutoka gerezani, mpaka wafungwa wengine wote wa kisiasa nchini waachiwe huru bila masharti yoyote kwanza!” aliandika Sugu.
Duru zimeutafsiri ujumbe huo kama ni moja ya sharti la Lissu endapo mengine yaliyowahi kuelezwa kama msimamo wa Chadema ikiwa pamoja na tume huru itakayotoka nje ya nchi yenye kuaminika kuchunguza matukio ya tarehe 29 Oktoba .
Msimamo mwengine wa chama hicho ni pamoja na familia kupewa miili ya ndugu zao waliouawa kwenye maandamano ya 29 Oktoba.
Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini yenye namba 19605 ya mwaka 2025, akidaiwa kutoa maneno ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025, jijini Dar es Salaam, akiwa raia wa Tanzania mwenye utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maneno ya kuitishia Serikali na kuonesha nia hiyo kwa kuchapisha meneno hayo katika mitandao ya kijamii kuwa:
“Wakisema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli…, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, hivyo ndivyo namna ya kupata mabadiliko…, kwa hiyo tunaenda kukinukisha…, sana sana huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga kwelikweli…, tunaenda kukinukisha vibaya sana…”
Kesi hiyo inayosikilizwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Iringa, Dunstan Ndunguru akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
ZINAZOFANANA
Tume ya Rais Samia yapingwa kila kona
Mtanzania aliyeuwawa na Hamas arudishwa Tanzania
Rais Samia aunda Tume ya kuchunguza matukio ya 29 Oktoba