MWILI wa Joshua Loitu Mollel (21), raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeuawa na kundi la wanamgambo wa Hamas, wakati wa mauaji ya tarehe 7 Oktoba mwaka 2023, unatarajiwa kuwasili leo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, mwili wa Joshua, utawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kutokea nchini Israel, ambapo utapokelewa na familia yake na mamlaka ya serikali.
Mapema jana, Ubalozi wa Tanzania nchini Israel ulifanya ibada ya katika mnara wa kumbukumbu wa Tel Aviv kabla ya kuondoka kwa mwili huo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Alex Kallua.
Joshua Mollel alikuwa akifanya mafunzo ya kilimo kusini mwa Israel wakati watu wenye silaha wakiongozwa na Hamas waliposhambulia eneo hilo, 7 Oktoba 2023.
Mwili wa Joshua ulikabidhiwa kwa serikali ya Israel, kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na majeshi ya taifa hilo.

Joshua aliuawa huko Kibbutz Nahal Oz, na mwili wake baadaye ukachukuliwa na washambuliaji.
Israel imekabidhi miili ya Wapalestina 285 badala ya miili ya mateka 19 wa Israel iliyorejeshwa na Hamas, pamoja na ile ya mateka watatu wa kigeni, mmoja wa Thai, Nepal na Tanzania.
Kundi hilo limetawala Ukanda wa Gaza kwa takriban miaka 20, likiowangoza Wapalestina wapatao milioni mbili kwa mkono wa chuma na kupigana na Israel mara kwa mara.
ZINAZOFANANA
Rais Samia aunda Tume ya kuchunguza matukio ya 29 Oktoba
Maandamano ya Gen Z kuikosesha Tanzania mabilioni
Mwanajeshi wa Marekani akamatwa na mabomu Tanzania