November 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mwigulu kuapishwa kesho Ijumaa

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba

 

WAZIRI mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano, Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuapishwa kesho, saa saba mchana, Ikulu mjini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, imeeleza kuwa Mwigulu ataapishwa na Samia Suluhu Hassan, kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kesho tarehe 14 Novemba 2025.

Jina la Mwigulu, limethibitishwa na Bunge la Tanzania, leo tarehe 13 Novemba 2025, muda mfupi baada ya kuwasilishwa na rais.

Hafla ya uapisho wa waziri mkuu huyo mteule itafanyika Ikulu ya Chamwino, majira ya saa saba mchana.

Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (50), amethibitishwa kwa kura 369 za ndio kati ya 371 zilizopigwa. Kura mbili zimeharibika.

About The Author

error: Content is protected !!