November 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Lissu apinga shahidi wa siri kutoonekana na majaji

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeshtakiwa kwa tuhuma za uhaini kwenye Mahakama ya Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, amepinga namna ya utolewaji wa ushahidi wa mashahidi wa siri kwenye kesi inayomkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 12 Oktoba 2025, mbele ya jopo la majiji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Iringa, Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde upande jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga liliwasilisha shahidi wanne aliyetambulishwa mahakamani hapo kuwa ni shahidi wa siri aliyepewa jina la uficho P11.

Lissu alidai mahakamani hapo kuwa pamoja kuwa shahidi huyo wa kificho lakini kanuni zinataka shahidi huyo aonwe na mahakimu au majaji wanaosikilizwa.

“Sasa nina pingamizi, waheshimiwa majaji huyo shahidi wa siri anatakiwa asimame kwenye kizimba na sio huko ambako haonekani.

“Napenda kuwafahamisha kwamba hili suala la ulinzi wa mashahidi, nimelitafakari kwa zaidi ya miezi 6 sasa na nimeliangalia kwa makini sana,” amedai Lissu.

Lissu amedai mahakamani hapo kuwa, hakuna shahidi yoyote kwa amri iliyotolewa na mahakama hakuna shahidi hata mmoja ambaye anatakiwa kutoa ushahidi akiwa kwenye kificho badala yake anatakiwa akae kizimbani.

“Naomba nianze na sheria sasa kwamba inasema nini kuhusu hawa wanaoitwa Mashahidi wa siri”

“Kanuni za ulinzi wa mashahidi za Mwaka 2025, zimeeleza hicho kiboksi hapo ni kitu gani kisheria”

Lissu amedai kuwa kanuni ya tatu ya ya sharia ya kulinda mashahidi inataka kuwepo kwa kizimba maalum ambacho anatakiwa aonwe na hakimu au jaji.

“Nasisitiza isipokuwa kwa Jaji au Hakimu. Sasa swali Je hapo alipokaa shahidi waheshimiwa majaji mnaweza kumuona huyo shahidi?” alihoji Lissu.

“Waheshimiwa majaji kwa macho yangu shahidi hapo haonekani kwa majaji, wala mimi simuoni. Watu pekee wanamjua ni hawa mawakili wa serikali waliomleta akina Katuga” aliongoza Lissu.

Lissu amehoji “kwa misingi gani ya haki katika dunia hii?

About The Author

error: Content is protected !!