
MAHAKAMA Kuu Masjala Kuu Dodoma imeitupa kesi ya Luhaga Mpina na ACT-Wazalendo, ikieleza kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) haipaswi kuingiliwa na chombo chochote kwa jambo ambalo ilifanya kwa nia njema. Anaripoti Zakia Nanga, Dodoma … (endelea).
Mpina alikuwa akipinga kuenguliwa katika nafasi ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano tarehe 15 Oktoba 2025 mbele ya mahakama hiyo na kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo Jaji Fredrick Manyanda. Majaji wengine waliosikiliza kesi hiyo ni Sylvester Kainda na Abdallah Gonzi.
Kwa uamuzi huo, Mpina hataweza kushiriki kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu, ambao kwa sasa vyama vya siasa vinavyoshiriki vinaendelea na kampeni.
ZINAZOFANANA
Lissu hajamalizana na shaihidi wa serikali, msiba waahilisha kesi yake
Raila Odinga afariki dunia
OMO aahidi kupitia upya mfumo wa mafao ya wastaafu serikalini