HUKUMU ya kesi ya Luhaga Mpina dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) itasomwa tarehe 10 Oktoba 2025. Anaripoti Zakia Nanga, Dodoma … (endelea).
Kesi hiyo namba 23617, ipo mbele ya majaji watatu wakiongozwa na Frederick Manyanda , Abdallah Gonzi na Sylvester Kainda.
Leo Jumatatu tarehe 6 Oktoba 2025 Mpina amefika mahakamani akiongozana na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mbarala Maharagande.
Katika maelezo yake Jaji Manyanda amesema ni muhimu hukumu hiyo ikatolewa mapema kutokana na unyeti wa shauri hilo.
ZINAZOFANANA
Mwanasheria wa kimataifa ataka Tanzania isifukuzwe Jumuiya ya Madola
Mwabukusi amuonya RC Chalamila, amtaja sakata la 29 Oktoba
Mabalozi wa magharibi wataka uchunguzi huru wa mauaji ya 29 Oktoba