
MAHAKAMA Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa aliyopewa Tundu Lissu anayeshtakiwa mahakamani hapo kwa tuhuma za uhaini iliyohusu tarehe ya hukumu ya shauri hilo ilhali haijaanza kusikilizwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)
Mchana huu Jaji Dunstan Ndunguru aliyeongoza jopo la majaji watatu kwenye shauri hilo amesema kuwa kesi hiyo inaweza kuiha kabla ya siku 30 au zaidi ya siku hizo.
Kuhusu kuzuiliwa kwa ndugu, marafiki na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho Lissu ndio Mwenyekiti wake mahakama imesema kuwa ilishatoa maelekezo yanayopaswa kutekelezwa na msajili wa mahakama hiyo.
Jaji Nduguru amesema kuwa kuhusu kikao cha kabla ya shauri ni kikao cha kawaida kinachotaka mrejesho wa yaliyokamilika na yale yasiyokamilika kwenye mwenendo wa mashauri.
Baada ya kutoa ufafanuzi huo Wakili wa Serikali Mkuu Lenatus Mkude alisimama na kudai kuwa upande wa Jamhuri umefika na shahidi wake ambaye ni Ofisa wa Jeshi la Polisi , ASP George Wilbard Bagyemu (48) .
ZINAZOFANANA
Msaidizi wa Mafwele aanza kutoa ushahidi kesi ya Lissu, kesho zamu yake kumbanwa
Mawakili wa Polepole watoa tamko
Lissu asimamisha mahakama kisa tarehe ya hukumu yake kabla ya kusikilizwa