
Onesmo OleNgurumwa, Mratibu wa THRDC-Taifa
MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC) umetoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa maridhiano na kupatikana kwa muafaka wa kitaifa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mapendekezo hayo yametolewa leo tarehe 5 Oktoba na Mratibu wa mtandao huo Onesmo Olengurumwa alipokuwa akitoa ripoti ya namna ilani za vyama vya siasa lilivyoweka kipaumbele suala la katiba mpya.
Olengurumwa amesema kuwa kabla ya yote kuundwe kamati ya makundi mbalimbali nchini itakayokuwa kamati ya muafaka wa kitaifa kwa ajili ya kuwaweka Watanzania wote pamoja.
“Suala hilo sio la kisiasa hivyo washirikishwe wananchi wote kwa makundi mbalimbali kamati hii itafanyika kazi mpasuko uliotokana na masuala ya siasa nchini,” amesema Olenhurumwa.
Amesisitiza suala la katiba mpya litangulie mapema baada ya uchaguzi mkuu mwaka mmoja na mchakato uishe mwaka huo huo.
ZINAZOFANANA
JWTZ yaonya wanaojaribu kulihusisha na siasa
Mahakama yaombwa kibali cha kuwakamata Viongozi wa Chadema
Zitto awapigia magoti wananchi wa Kigamboni kumchagua Mndeme