October 3, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Zitto awapigia magoti wananchi wa Kigamboni kumchagua Mndeme

 

KIONGOZI wa Chama (KC) mstaafu cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amewataka wananchi wa jimbo la Kigamboni, kumpigia kura mgombea ubunge wa chama chake, Mwanaisha Mndeme. Anaripoti Ulwe Rajabu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, hakuna mgombea yoyote wa ubunge katika jimbo la Kigamboni, kutoka chama chochote cha siasa, anayeweza kuliongoza jimbo hilo na kufanyia kazi changamoto zilizopo, nje ya mgombea wa chama chake.

Alitoa kauli hiyo, leo tarehe 2 Oktoba 2025, wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake wa hadhara katika Kata ya Kimbiji. Kabla ya mkutano huo, Zitto alifanya ziara maalum katika jimbo hilo, kwa ajili ya kumnadi rasmi Mndeme.

Mbali na kunadi Mndeme, kiongozi huyo mkuu wa ACT-Wazalendo, alinadi wagombea udiwani wa kata mbalimbali katika jimbo hilo.

Naye Mdeme, mwanasiasa na Wakili wa Mahakama Kuu, akizungumzaa katika mikutano hiyo, aliahidi wananchi kuleta uwakilishi na imara.

Kupitia ziara hii, wananchi wa Kigamboni wamepata fursa ya kusikiliza sera mbadala zinazolenga kuondoa changamoto za muda mrefu na kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

ACT -Wazalendo inaendelea kusimama kidete kwa ajili ya usawa, uwajibikaji na maendeleo jumuishi kwa Watanzania wote, amekuwa akieleza Mndeme katika mikutano yake.

About The Author

error: Content is protected !!