October 3, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TCU yaongeza siku nne za udahili

Profesa Charles Kihampa

 

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kuongeza muda wa udahili kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kwa kuweka awamu ya tatu na yamwisho anayotarajiwa kufunguliwa tarehe 6 Oktoba , na kufungwa tarehe 10 Oktoba, mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamaelezwa leo tarehe 3 Oktoba 2025 na Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa kupitia taarifa yake iliyowekwa kwenye tovuti hiyo imeeleza kuwa majina ya waombaji waliopata nafasi katika awamu ya pili yatatangazwa na vyuo husika kuanzia tarehe 6 Oktoba 2025.

Kwa mujibu wa taarifa hio ongezeko la muda linalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioomba katika vyuo zaidi ya kimoja na ambao hawakuthibitisha nafasi zao katika awamu ya kwanza.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa waombaji waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja katika awamu ya pili, pamoja na wale ambao hawakuthibitisha nafasi zao awali, wanapaswa kuthibitisha chuo wanachokusudia kusoma kati ya tarehe 6 hadi 19 Oktoba 2025.

“Uthibitisho huo utafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu au barua pepe wakati wa maombi. Kwa wale watakaoshindwa kupokea ujumbe huo kwa wakati, TCU imewaelekeza kuwasiliana na mifumo ya udahili ya vyuo husika ili kupata msaada,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha TCU imeeleza kuwa orodha kamili ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja itapatikana kwenye tovuti ya Tume (www.tcu.go.tz) kuanzia tarehe 6 Oktoba.

About The Author

error: Content is protected !!