
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
DIMTRY Peskov, msemaji wa Ikulu ya Urusi, ameituhumu Marekani kuchochea vita nchini Ukraine. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Peskov anasema, “Acha kuchochea vita. Usitulazimishe kuendeleza mashambulizi yake yetu dhidi ya Ukraine.”
Kauli ya mwanasiasa huyo, imekuja muda mfupi baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kueleza kuwa Ukraine inaweza kurudisha maeneo yake yote yaliyochukuliwa na Urusi kwa kile alichoeleza, “kwa kuwa sasa uchumi wake umedorora.”
Trump amesema, Kyiv inaweza “kushinda Ukraine yote na kuirejesha katika hali yake awali,” jambo ambalo limeashiria mabadiliko makubwa katika msimamo wake kuhusu vita vyake na Urusi.
Katika chapisho kwenye jukwaa lake la la kijamii, Truth Social, Trump amesema, Ukraine inaweza kurudisha “mipaka ya asili kutoka mahali ambapo vita hivi vilianza” kwa msaada wa Ulaya na Nato, kutokana na shinikizo kwa uchumi wa Urusi.
Maoni yake yamekuja baada ya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, yaliyofanyika baada ya kiongozi huyo wa Marekani kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York.
Trump amerudia kuelezea nia yake ya kumaliza vita, lakini hapo awali alionya kwamba mchakato huo unaweza kuhusisha Ukraine kutoa eneo fulani, matokeo ambayo Zelensky amekuwa akiyakataa mara kwa mara.
Rais Zelenskyy ameendelea kusisitiza kwamba mtu pekee anayeweza kubadilisha hali ya mambo katika vita hivyo ni Trump.
Amesema, “Trump ni mtu anayeweza kuubadili mchezo peke yake, ikiwa atakuwa na uhakika na Ukraine. Na nadhani yuko karibu zaidi na hali hii, na ndiyo sababu kati yetu, ni Trump pekee anayeweza kubadilisha hali.
“Kwa leo, tunawajua wachache, sio watu wengi sana duniani ambao wanaweza kubadilisha mchezo. Lakini yeye ndiye yuko karibu zaidi na hili” alieleza Zelenskyy.
Lakini Kremlin imesisitiza kuwa Ukraine haina uwezo huo.
ZINAZOFANANA
Rais wa Malawi akubali kushindwa
Changamoto za afya barani Afrika zitatatuliwa na CDC
Chakwera adai ana ushahidi wa kura za wizi