September 23, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Chakwera adai ana ushahidi wa kura za wizi

 

CHAMA Tawala cha Malawi Congress kinachoongozwa na Rais Lazarus Chakwera (MCP), kimedai kina ushahidi juu ya Kura za Wizi, wakati ambapo matokeo ya awali yanaashiria kuwa kinaelekea kupoteza Madaraka katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Vitumbiko Mumba ambaye ni Mgombea Mwenza wa Rais Chakwera, amesema wana ushahidi unaoonesha watu wakijaza Karatasi Bandia za kupigia kura kwenye masanduku ya kura.

Hadi sasa kwa mujibu wa taarifa za awali, Matokeo ya Kura yanaonesha Rais wa zamani, Peter Mutharika anaongoza kwa zaidi ya 51% ya Kura akifuatiwa na Rais wa sasa, Lazarus Chakwera mwenye 39%.

Mumba amesema chama cha MCP, kimewasilisha malalamiko yake katika Tume ya Uchaguzi (MEC) ambapo Tume hiyo ina muda wa hadi Septemba 24, kuwa imetangaza matokeo rasmi ya Urais.

Kauli ya Netanyahu imeibua mjadala mkubwa wa kimataifa, hasa ikizingatiwa kuwa nchi zilizotangaza kutambua Palestina zimesema hatua hiyo inalenga kuhimiza suluhisho la amani la mataifa mawili na kusaidia Wapalestina kupata haki yao ya kujitawala.

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amepongeza hatua hiyo, akiita ni hatua muhimu kuelekea haki, uhuru na amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati.

About The Author

error: Content is protected !!