
MIILI ya masista wanne wa Shirika la Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, waliofariki kwenye ajali ya gari jijini Mwanza, imeagwa leo kwenye ibada ya misa iliyofanyika Parokia ya Mwenyeheri Isidori Bakanja – Boko, jimbo la Bagamoyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Ibada hiyo ambayo iliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule iliongozwa na Askofu Eusebius Nzigilwa.
Katika wanne hao watatu ambao ni Mama Mkuu wa Shirika hilo sister Nelina Semeoni (60) raia wa Italia, Sister Damaris Matheka (51), Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bukumbi na raia wa Kenya na Sister Stellamaris Kamene (48), walizikwa kwenye Bustani lililopo kwenye eneo la shirika hilo, huku mwili Sister Lilian Kapongo (55) ukisafirishwa kuelekea mkoani Tabora.
Wanne hao walifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Bukumbi, wilayani Misungwi, mkoani Mwanza. Tarehe 15 Septemba 2025, majira ya saa 1 usiku.
Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Chalamila, pamoja na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule walitoa kiasi cha shilingi milioni 10 kama rambirambi kufuatia vifo hivyo.
ZINAZOFANANA
Meridianbet yaendeleza harakati za usafi hospitali ya Mwenge
Wengine wawili wafariki dunia kwenye ajali ya basi na lori
Polepole awapa somo jipya polisi