
Frank Nyalusi
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika wilaya ya Iringa Mjini, Frank Nyalusi, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa, tarehe 19 Septemba 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho na familia zinasema, Nyalusi amekutwa na mauti katika hospitali ya Rufaa ya mkoani wa Iringa, alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa akipatiwa matibabu.
Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, John Heche, amemueleza marehemu Nyalusi kama mpiganaji asiyechoka.
Anasema, “Nyalusi alikuwa hasubiri kutumwa na chama. Alikuwa anajituma. Alikuwa hasubiri maelekezo. Alikuwa anaelekeza yeye. Kwa kweli, chama chetu kimepoteza mtu muhimu, jasiri na mahiri.”
Naye Mchungaji Peter Msigwa, aliyewahi kuwa mbunge wa Chadema, katika jimbo la Iringa Mjini, kati ya mwaka 2010 na 2020, amesema amepokea kwa mstuko mkubwa taarifa ya kifo cha Nyalusi.
Akiandika kupitia ukurasa wake wa x zamani twitter, Msigwa amesema, “Rest in peace mdogo wangu. Life will never be same4 without you! Jana nilijaribu kuja kukuona jioni. Bahati mbaya sikuruhusiwa kwa kuwa ulikuwa ICU.”
Ameongeza, “Kwa heri Nyalusu. Wewe ni sehemu ya historia ya maisha yangu. Tumefanya siasa kwenye shida na raha, nitakukumbuka sana.”
“Kwa masikitiko makubwa tunapenda kutoa taarifa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Mwenyekiti wetu wa wilaya ya Iringa Mjini, Frank John Nyalusi, kwamba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo,” imeeleza taarifa ya Chadema, katika wilaya yake.
Taarifa imeongeza: “Mwenyezi Mungu akampe pumziko la milele. Akawe mfariji kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki na wanachama wote wa Chadema.
“Tunamshukuru Mungu kwa maisha yake hapa duniani. Mbele yake nyuma yetu. Hakika vita umevipiga na mwendo umeumaliza tutaonana baadae kaka wa wote.”
Frank John Nyalusi, alikuwa nguzo muhimu ya Chadema katika jimbo la Iringa na kwamba alikuwa mmoja wa waliochochea mabadiliko ya uongozi ya chama hicho, katika uchaguzi mkuu wa 21 Januari mwaka huu.
Uchaguzi mkuu wa 21 Januari, uliomuweka madarakani Tundu Lissu na kumaliza ukoloni wa Freeman Mbowe ndani ya Chadema, unabaki kuwa kumbukumbu ya historia ya Nyalusi ya kuchagiza mabadiliko kwenye chama chake.
ZINAZOFANANA
Wahenga aahidi maturubai Kinyerezi
Hatma kesi ya Lissu kujulikana Sept 22
Polepole awapa somo jipya polisi