
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi, Jaji Annabel Mtalimanja
VYAMA viwili vya siasa nchini Malawi – Malawi Congress Party (MCP) na Democratic Progressive (DP), vimejitangaza washindi wa kiti cha urais nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi, Jaji Annabel Mtalimanja amesema, mchakato wa kuhesabu kura haujakamilika na kuwaonya wanaojitangaza washindi bila ridhaa ya tume.
Katika uchaguzi huu, MCP imemsimamisha Peter Mutharika na DP, mgombea wake, alikuwa Lazarus Chakwera, rais wa sasa wa taifa hilo.
Jaji Mtalimanja amesema, tume yake haitaharakisha mchakato wa kuhesabu kura na amevitaka vyama na wagombea kuheshimu mchakato na taratibu za kutangaza matokeo.
Uchaguzi mkuu wa Malawi unaochagua rais, Bunge na mabaraza ya mitaa, ulifanyika Jumanne iliyopita. Umekuwa na ushindani mkali kati ya Rais wa sasa, Lazarus Chakwera na mtangulizi wake, Peter Mutharika.
Chakwera na Mutharika, walikutana katika uchaguzi uliyopita, ambapo rais wa sasa alimuondoka madarakani mshindani wake huyo.
Zoezi la kuhesabu kura lilianza mara baada ya muda wa upigaji kura kukamilika kwenye nchi hiyo iliyokubwa na kuporomoka kwa uchumi wake na ongezeko la umaskini.
Wachambuzi na waangalizi wa kimataifa wanasema, kuna uwezekano mkubwa wa Mutharika kuibuka na ushindi, ingawa Chakwera naye ameeleza kuwa ana matumaini ya ushindi.
George Chaima, mchambuzi wa siasa nchini humo amenukuliwa akisema, matokeo ya awali, yanaonyesha wananchi wa Malawi wanamuunga mkono Mutharika kurejea madarakani, kwa maelezo kuwa chini ya uongozi wake (2014 hadi 2020), taifa hilo lilikuwa bora zaidi.
Malawi Congress Party (MCP), chama kikongwe nchini Malawi, kilichoongozwa na Dk. Hastings Banda, kinaingia madarakani na kutoka. Kiliwahi kujigeuza mkoloni mweusi.
Baada ya mwisho wa udikteta wa Banda, MCP ilizidi kushindwa katika uchaguzi, lakini kimekuwa kikijiimarisha na kurejea madarakani na kuendelea kuwa chama muhimu katika siasa za Malawi.
ZINAZOFANANA
ATCL yatangaza safara ya Dar-Lagos kwa dola 850
Rais wa zamani wa Brazil ahukumiwa mika 27 jela
Félicien Kabuga kurejeshwa Rwanda?