September 15, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Jeshi la Polisi liwaachie wale wote waliokamatwa Mahakamani leo

 

MWENYEKITI wa Chadema Kanda ya Pwani Boniface Jacob, amelaani vikali tukio lililofanywa na jeshi la Polisi kwa wanachama wa chama hicho waliofika Mahakamani kufuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Kiongozi huyo ameyasema hayo leo tarehe 15 Septemba 2025, mara baada ya kuahirishwa kwa shauri kwenye Mahakama kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Boniface amesema kuwa, mara zote wafuasi wa chama hicho wanapokuwa wenyewe kumekuwa hakuna shida, lakini ukiona tatizo basi jeshi la Polisi ndio huwa changamoto.

“Nafikili nyinyi waandishi wa Habari ni mashuhuda pamekuwa na amani, Chadema tumekuwa waungwana mara zote vurugu zinapotokea Polisi ndio wameanzisha lakini tukiachwa watu wakiwa wanakuja na kuondoka Chadema tumekuwa hatuna shida,” alisema Boniface.

Aidha katika hatua nyingine kiongozi huyo ambaye pia ni mjumbe wa kamati Kuu amelaani vikali tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema Taifa (Bavicha) Wakili Deogratius Mhinyila, na kulitaka jeshi la Polisi kuwaachia wale wote waliokamatwa hii leo Mahakamani hapo.

“Leo asubuhi limetokea tukio ambao sio la kiungwana na tunalilaani vikali kupingwa na kushambuliwa kwa Mwenyekiti wetu wa Bavicha, Deogratius Mhinyila ndani ya viunga vya Mahakama kwa wasiofahamu pana Kinga ya Mahakama ndio maana muharifu akiachiwa anakamatiwa nje.

“Lakini leo katika mazingira ya kuonekana ni kisasi, au kuwindwa kwa makusudi askari wamemshambulia na kumdhuru Mwenyekiti wetu ambaye ni Wakili wa Mahakama Kuu,” amesema Boniface.

About The Author

error: Content is protected !!